Advertisement

Breaking

Wednesday, November 23, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 43 & 44

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
Kwanza kijana huyo akamkumbatia raisi Praygod Makuya, nakumfanya raisi Praygod Makuya kujitahidi kuvuta kumbukumbu zake niwapi alipo muona kijana huyu anaye mwagikwa na machozi. Kumbukumbu za raisi Praygod Makuya zikagota kwenye ndege na kukumbuka kijana huyu ndio yule aliye kuwa akishirikiana na Rahab.
“We…weee si…”   
Raisi Praygod alizungumza kwa kigugumizi, kwani kama kijana huyu alimkosa kwenye ndege basi leo amekuja kumuua kwenye alaiki ya watanzania.
“Samson, Samson muheshimiwa.”
Samson alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika, akazidi kumkumbatia Raisi Praygod Makuya kwa nguvu zake zote.
                                                                                         
ENDELEA
Raisi Praygod Makuya akajaribu kujitoa mikoni mwa Samson ila akajikuta akishindwa kwani Samson alizidi kumkumbata kwa nguvu
“Naoamba unisamehe muheshimiwaa”
Samson alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi. Makamu wa rais baada ya kumuona Samson, ikanyanyuka kwenye kiti chake huku macho yakiwa yamemtoka. Woga wa siri yake kuweza kufichuliwa na mjomba wake huyo ukaanza kumtawala. 
“Muheshimiwa natambua kwamba nilikukosea, ila si kosa langu mimi”
“Nilitumwa niweze kukuangamiza, na mjomba wangu ili kiti chako cha uraisi kiweze kukaliwa na mjomba wangu ambaye ni makamu wa raisi wa sasa”
Maneno ya Samson yakamfanya raisi Praygod kuweza kumtazama makumu wa raisi aliye  keti kwenye jukwaa. Sura ya makamu huyo ikamuashiria raisi Praygod kwamba ina hasira dhidi yake. 
“Nimekuelewa kijana, unaitwa nani?”
“Samson”
“Sawa Samson nitalifanyia kazi”
“Kabla ya hayo kuna jengine muheshimiwa nahitaji kukuambia”
Makamu wa raisi alipo zidi kumuona Samson anazungumza na Raisi Praygod, akazidi kushikwa na hasira akiamini kwamba kila kitu kimesha haribika, akaangaza macho yake huku na huku, akamuona mlinzi wake aliye simama pembeni, bastola ikiwa imechomekwa kiunoni. Kwa haraka makamu wa Raisi akaichomoa bastola hiyo bila hata yakufikiria mara mbili, akafyatua risasi ambazo kwa haraka Samson aliweza kuliona tukio hilo, alicho kifanya ni kumsukumia pembeni Raisi Praygod, na risasi hizo mbili zikaingia mwilini mwake na kumuangusha chini.
Mlio wa bastola hiyo, ukazua hali ya taharuki kwa kila aliye kuwa katika uwanja wa taifa, kila mmoja akafanya jinsi akili yake ilivyo muagiza kuweza kufanya, wapo walio weza kuchanganya miguu yao na kukimbia hovyo hovyo, wengine waliweza kupoteza fahamu, wengine waliweza kukanyagwa vibaya pale walipo zidiwa nguvu na wale walio hitaji kuokoa nafsi zao. Askari na walinzi wa viongozi waalikwa wakawa na kazi moja tu, yakuwaokoa viaongozi wao waliomo ndani ya kiwana hichi kikubwa cha mpira. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani hapakuwa na aliye weza kuvumilia. Walinzi wengi wakamzunguka Raisi Praygod, wakamtoa uwanjani huku wakiwa wanamkimbiza, baadhi ya wanajeshi wakaweza kumtia nguvuni makamu wa raisi aliye weza kufanya tukio lakinyama.
Hali ya Samson, ikazidi kuwa mbaya huku macho yake akimtizama jinsi Raisi Praygod anavyokimbizwa na askari kuyaokoa maisha yake, Samson akaachia tabasamu pana, huku taratibu macho yake yakiingiwa na ukungu ulio pelekea kuyafumba macho yake na kutulia tuli.
                                                                                         ***
     Moja kwa moja Agnes akakimbilai kwenye chumba amacho aliamini kiongozi anaye muhitaji ni lazima atakuwa amepelekwa huko baada ya milipuko hiyo ya magari kuweza kutokea. Akafanikiwa kufika kwenye kordo yakuelekea kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi. Walinzi walio valia suti nyeusi pamoja na miwani nyeusi wapatao kumi na tano, wakawa wamesimama nje ya mlango huo huku macho yao yote wakimtupia Agnes anayekuja kwa kasi huku akiwa amejiamini sana. 
Kila mmoja akabaki kuwa na alama ya kujiuliza kwani mavazi aliyo yavaa Anges ni ngumu sana kumtilia mashaka kwani akafanana sana na wahudumu wa kikosi cha kuzima moto. Muonekano wa umbo dogo dogo la Agnes, likawapa imani kwamba binti huyo anaye kuja kasi huku akiwa amenyanyau mikono yake juu, hana madhara yoyote kwao.
“Naomba muwatoe viongozi nje, jengo limeanza shika moto”
Kauli ya Agnes aliyo izungumza kwa lugha ya kirasia, ikawafanya walinzi wote kuchanganyikiwa, ikawalazimu kuwasiliana na wezao waliomo ndani ya chumba kuweza kuwatoa viongozi hao haraka iwezekanavyo. Bwana Paul Henry Jr pamoja na Raisi wa Russia wakatolewa ndani ya chumba hicho kuku wakiwa wamezungukwa na walinzi wao wapatao ishirini.
“GO GO GO….!!!”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akionekana ndio mkuu wa kikosi hichi maalumu chakuwalinda viongozi hawa. Agnes akatazama jinsi walinzi hawa walivyo makini na kuwalinda viongozi hawa.
“Hapa hapa”
Agnes akawaacha viongozi hao kupiga  hatua nyingi mbele, kisha  kwa kasi akanza kukimbia na kuwafwata kwa nyuma, akamfikia mmoja aliye ishika bastola yake na kuitanguliza mbele. Kwa kasi ya ajabu Agnes akajigeuza kwenye shingo ya mlinzi huyo na kuivunja, kabla hajaanguka chini, tayari akawa ameikamata bastola ya mlinzi huyo. 
Kwa mafunzo ya uharaka na umahiri wake katika kutumia silaha hizi za bunduki, Agnes, akaanza kuwaangusha chini walinzi hao, walio changanyikiwa kwani, kitendo cha mtu kujaribu kufanya shambuliza tayari umesha vamiwa na kuangushwa chini.
Agnes akafanikiwa kusimama nyuma kwa bwana Paul Henry Jr, akampiga kabali huku bastola yake akiwa ameiweka sikioni mwa kiongozi huyo. Macho yake kwa haraka aliweza kuona miili ya walinzi wapatao kumi na sita wakiwa chini wamekufa huku wanne wakiwa wamesimama huku wamenyooshea bastola zao.
Rasi wa Russia hakuweza kuamini uwezo aliokuwa nao msichana mdogo kama huyo aliye anzisha varangati la kufa mtu na kuwaweka chini watu wazima na kuwa kimya.
“Nipisheni”
Agnes alizungumza kwa kujiamini, kiasi kwamba hapakuwa na mlizi aliye weza kufanya kitu chochote. Askari na kikosi cha zima moto nje wakawa na kazi moja ya kuendelea kuwasogeza watu wasiweze kuingia ndani ya hoteli hii kwani ni hatari kwa maisha yao. Hapakuwa na askari aliye weza kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea huko ndani.
“Binti tutakupa chochote ili mradi umeachie huyo kiongozi”
Raisi wa Russia alizungumza huku akiwa anatetemeka sana, Agnes hakuhitaji kumsikiliza hata kidogo, akampiga risasi ya mguu raisi huyo, akamfanya aanguke chini na kutoa ukelele mkali wa maumivu, walinzi wake wakiwa katika mawenge mawenge, Agnes akajaribu kufyatua risasi, akagudua risasi zilizomo ndani ya bastola yake zimekwisha. Agnes akiwa katika hali ya kuishangaa mlinzi mmoja akawa amefanikiwa kuligundua hilo.
                                                                                            ***
       Raisi Praygod akingizwa kwenye gari, akapelekwa moja kwa moja Ikulu, kwa ajili ya mapumziko huku askari wengine wakimpeleka makamu wa raisi katika kambi ya jeshi huku wakimuweka chini katika ulinzi mkali. Gari tano za jeshi zilizo jaa askari, zikajikuta zikifunga breki katika maeneo ya mwenge, baada ya kukuta foleni kubwa ya magari ya wananchi. 
Wanajeshi wapatao sita wakiwa na bunduki wakashuka kwenye magari hayo na kuanza kufanya kazi ya kuwaamrisha wenye magari yao kuweza kuyasogeza pembeni, ikiwa ni amri na si ombi, kwani wanamualifu mmoja waliye hakikisha kwamba hachomoki kwenye mikono ya serikali kwani ameshababisha maafa makubwa kwa raisi pamoja na viongozi walio weza kuingia katika uwanja wa mpira wa taifa.
Gari mbili nyeusi aina ya VAN, zikasimama katikati ya sehemu ambayo magari hayo yalipaswa kuweza kupita. Wakashuka vijana watatu walio valia mavazi meusi pamoja na vinyago usoni mwao. Kila mmoja akiwa na bunduki aina ya AK47
Hapakuwa na aliye weza kuuliza, walicho kifanya ni kuanza kuwashambulia wanajeshi wote walio weza kutoka nje ya magi yao, wakihitaji kuweza kupishwa na waendelea na msafara wao. Kila raia aliyekuwa ndani ya gari liwe lake au daladala, waliweza kuchomoka kila mmoja kuyaokoa maisha yake. 
Vijana hao walio valia sura za vinyago hawakuwa na woga wa ana yoyote, walizidi kusonga mbele kwenda zilipo gari za jeshi. Wanajeshi waliomo ndani ya magari, wakajirusha nje huku kila mmoja akiwa ameikamata bunduki yake sawia kuhakikiusha kwamba wanapambamba vilivyo hadi dakika ya mwisho.
Hapakuwa na alie jua kuwa wavamizi hao wanajiamini kwa kitu gani, kwani waliweza kusonga mbele pasipo kuogopa, wanajeshi walio jibanza kwenye magari yaliomo barabarani, wakajikuta wakianza kuangushwa mmoja baada ya mwingine, huku risasi zinazo zidi kuwateketeza wasitambue ni wapi zilipo tokea.
                                                                                    
          SHE IS MY WIFE(44)

Wadunguaji, walenga shabaha ya masafa ya mbali wapatasi sita wakiwa wamesimama katika magorofa kadhaa yaliyopo katika makutano ya magari ya mwenge, waliweza kufanya kazi yao sawia, kila mwanajeshi aliye weza kuonekana maisha yake yaliondolewa kwa risasi za vichwa. 
“No one Clear”
“Two Clear”
“Three Clear”
“Four Clear”
“Five Clear”
“Six Clear”
Wadunguaji wote waliweza kuwasiliana kwa vifaa vyao maalumu vya kunasia sauti, huku kila mmoja akidai hakua mwanajeshi anaye onekana kwenye eneo hilo. Watau walo chini wakakimbia kwa haraka hadi sehemu zilipo gari za wanajeshi, wakafungua kari mmoja wakamkuta makamu wa raisi akiwa amefungwa pingu pamoja na kivishwa kipande cha gunia cheusi. Wakamfunua kipande hicho
“Muheshimiwa tupo hapa kwa ajili yako”
Mmoja alizungumza kwakujiamini na kumfanya makamu waraisi kuweza kutabasamu. Mlio wa helcoptar ukasikika, mmoja akatoka nje ya gari hilo. Akawasiliana na wezao waliomo ndani ya helcoptar hiyo, ambayo kwa uwezo wake mkubwa, ikaweza kushuka karibu sana na eneo ambalo gari hilo lipo. Makamu wa raisi akatoka ndani ya gari akadandia ngazi aliyo teremshiwa na kuanza kuiparamia hadi juu. Wavamizi hao watatu nao wakapanda kwenye helcoptar kwa kutumia vingazi hivyo walivyo shushiwa kisha wakaondoka zao katika eneo la tukio.
   ***

“Shitii”
Agnes alizungumza, akamsukumia bwana Paul Henry Jr mikononi mwa walinzi wake hao watano, wakajaribu kumdaka kiongozi wao asianguke chini, hapo ndipo ikawa nafasi kwa Agnes kuchuchumaa kwa haraka chini, kunyanyuka juu mikono yake milili iliweza kuwa na bastola alizo ziokota chini kwa walinzi walio kufa. Hakuhitaji kufanya makosa. Akawaogesha walinzi hao mvua ya risasi wakabaki viongozi wawili Bwana Paul Henry Jr pamoja na Raisi wa Russia.
Jasho likiwa linamwagika usoni Agnes akamtizama kiongozi huyo wakimarekani, alicho kifanya, akafyatua risasi tano mfufulizo zilizo tua kifuani kwa kiongozi huyo bwana Paul Henry Jr na hapo ndipo ukawa mwisho wa maisha ya kiongozi huyo.
“Mission yangu ilikuwa ni kwa huyu wewe leo umepona”
Agnes alizungumza huku akiwa amemuinamia muheshimiwa Raisi, kwa kutumia kitako cha bastola akampiga nacho cha kichwa, raisi akazimia hapo hapo.
“Mission complite”
Agnes alizungumza huku akiitazama miili ya marehemu ali wapa tiketi ya kuwahi kwenda mbinguni siku ya leo. Kwa haraka akatoka katika eneo hilo lililopo chini ya ardhi, akatoka nje ya hoteli pasipo kujulikana, akakimbia hadi kwenye gari alilo acha kibeki chake, kwa bahati nzuri akafanikiwa kuweza kukiona. Akakichukua, akayavua mavazi ya zima moto, kisha akakimbia akiungana na wananchi wengine.
                                                                                        ***
“Madam tumeagizwa kuja kukuchukua kukupeleka ikulu”
Wanausalama wapatao wanne walisimama mbele ya Rahab, aliye toka usingizini asijue ni kitu gani kilicho weza kutokea.
“Nitaamini vipi nyingi ni watu wazuri”
Kila mmoja akatoa kitambulisho chake na kumuonyesha Rahab, vitambulisho vyao viliwaonyesha wao ni miongoni mwa walinzi wanao fanya kazi ndani ya ikulu. 
“Sawa twendeni”
Rahab akaagana wa waziri mkuu aliye jawa na huzuni usoni mwake, Rahab hakuhitajii kujua ni kiupi kinacho mfanya mama huyo kuwa katika hali kama hiyo. Akaingia ndani ya gari, huku macho yake akiwa amemkazia Sheila, taratibu gari zikaanza kuondola
‘Wewe mama huyu binti atakuja kukuliza siku’
Rahab alizungumza kimoyo moyo huku akiendelea kumuangalia Sheila ambaye alisha anza kujenga moyo wa chuki dhidi ya Rahab, mara baaya ya kuhisi kwamba Rahab anaweza kumuhitaji Eddy ambaye hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo. Wakafika ikulu salama salimi, Rahab akakutana na mumewe Raisi Praygod, ambaye kwa haraka alipo mtazama machoni mwake akatambua kuna kitu ambacho nikibaya kiliweza kutoka kwa mume wake.
Rahab akayafumba macho yake kwa haraka, hisia kali alizo weza kuwa nazo kwa kipindi hichi, zikaanza kumjia kichwani kwake, akayaona matukio yote yaliyojitokea masaa ya nyuma. Akazidi kuvuta hisia  ambazo zikampeleka hadi kwenye tukio la kijana aliye yaokoa maisha yake.
“HAHhahahaha….”
Rahab alistuka, huku akihema hii ni baada ya ya kuweza kuona mambo yakutisha kwa ambayo kijana huyo anaweza kuyafahamu vizuri na pasipo kuweza kuyazuia mapema basi nchi inaweza kuingia katika matatizo makubwa.
“Baby vipi unatatizo?”
Raisi Praygod alimuuliza Rahab baada ya kumuona anahema sana, huku macho yake kama yakiwa na uwekundu kama mtu aliye ingiwa na moshi mwingi wakuni.
“Nipo sawa tu”
“Twende chumbani kwanza”
Raisi Praygod akamuondoa katika eneo la sebleni Rahab, akampeleka chumbani kwake ambapo kwa rahab ndio mara yake ya kwanza kuweza kuingia katika chumbacho analala muheshimiwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania bwana Praygod Makuya.
“Mke wangu ninavikao vya dharura sijui unaweza kunisaidia kunisubiri kwa muda kadhaa”
Raisi Praygod alizungumza mara baada ya kumpandisha Rahab kitandani ili ajipumzishe
“Au nimuite doktar aje kukutibu”
“Hamna haja nipo sawa”
“Basi mke wangu ninaomba nielekee kwenye chumba cha mkutano”
“Usiku saa hizi”
“Ndio ni dharura”
“Sawa”
Raisi Praygod akainama na kumbusu mke wake mdomoni, kisha akatoka kwenye chumba hicho kwa haraka haraka akaelekea kwenye chumba cha mkutano ambapo alihitaki kuweza kukutanza na viongozi majeshi wote ilii kuweza kuhakikisha wanaiweka nchi katika hali ya usalama.
“Kilicho tokea muheshimiwa tunaomba utumiwe radhi kwani kikosi changu ndicho kilikuwa na jukumu la kuhakikusha makamu wa raisi anafika kwenye mikono ya ulinzi”
Mkuu mmoja wa jeshi la nchi kavu aliweza kuzungumza kwa niaba ya viongozi wengine wa jeshi. Raisi Praygod hakuzungumza kitu chochote zaidi ya macho yake kuyagandisha kwenye sehemu mmoja huku akijaribu kuyakumbuka maneno ya Samson
‘Kabla ya hayo kuna jengine muheshimiwa nahitaji kukuambia’
Kumbukumbu za Raisi Praygod zikakwamia hapo, akajikuta akiyafumba macho yake kwani hiyo ni ya jambo lililo muumiza kichwa.
“Jengine, Jengine lipi…………….?”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti iliyo wafanya wakuu wengine wote kumtazama, wasijue ni kitu gani ambacho muheshimiwa anakizungumza.
“Kuna yule kinaja ambaye alionikoa, fanyeni mawasiliano mujue ni wapi alipo sawa”
“Sawa mkuu”
“Hakikisheni munahimarisha ulinzi kila kona ya mipaka, viwanja vya ndege bahari pamoja na pengineo kwani bila kufanya hivyo hali itakuwa ni tete”
“Sawa muheshimiwa.”
“Muheshimiwa, yule kijana yupo Muhimbili anafanyiwa matibabu”
Secretary wa raisi alimnong’oneza raisi baada ya kupewa jukumu kukufwatilia ni pasi Samson alipo pelekwa.
Rahab hakuweza kufumba jicho laka na kulala, kitu alicho weza kukiona kwenye hisia zake kikamnyima raha, akatamani akiseme kwa mume wake, ila akahofia kuweza kutiliwa mashaka kwani tayari Rahaba amesha anza kujihisi kwamba yeye si mwanadamu wa kawaida. Rahab akanyanyuka kitandani, akaitupia macho saa ya ukutani inaonyesha ni saa saba kamili usiku, akiwa kaatika kuzunguka zunguka ndani ya chumba, mlango wa ndani kwake ukafunguliwa.
AkaingiaRaisi Praygod huku akionekana kuonakana kama mtu mwenye haraka ya kuhitaji kufanya jambo fulani.
“Munataa kwenda hospitalini?”
Rahab alimuuliza mume wake jambo lililo mfanya raisi Praygod kushangaa kidogo kwani jambo alilo liuliza mke wake hakuhitaji kumuambia.
“Umejuaje?”
“Wewe niambie tu kwani na mimi nahitaji kuonana na yule kijana”
“Unamfahamu?”
“Simfahamu ila ninakuomba tu mume wangu tuweze kwenda pamoja”
Raisi Praygod akamtazama Rahab usoni kwa sekunde kadhaa, kisha akakubaliana naye kwani hapakuwa na sababu ya msingi ya yeye kumkataza mke wake kwenda huko kwani anamtambua vizuri kwamba ni mpiganaji mzuri aliye weza kuyaokoa maisha yake kwa kiwango kikubwa sana.
“Jiandae”
Raisi Praygod alizungumza huku akisimama kwenye moja ya picha yake kubwa iliyo wekwa ndani ya chumba chake, akaitoa na kuiweka chini, hapo ndipo rahaba akagundua kwenye picha hiyo kuna mlango wa chuma, huku pembeni kukiwa na batani kadhaa ikashiria mlango huo unafunguliwa kwa namba za siri ambazo anazifahamu raisi peke yake.
Raisi Praygod hakuwa na wasiwasi wowote dhidi ya mke wake, akaingiza namba za siri, baada ya hapo akaweka kiganja chake pembeni ya namba hizo, kwenye kijikioo chenye usawa na kiganja chake. Mstari mwekundu ukapita mara mbili ukitokea juu kwenda chini, ukikagua kiganja hicho, baada ya kufanya hivyo mstari wa kijani ukaweza kupita ukitokea chini kwenda juu, na hapo mlango ukafunguka.
Raisi Prayogod akaingia kwenye chuma hicho chenye taa nyeupe tupu, Rahab hakutaka kubaki nyuma naye akaingia kuangalia ni kitu gani ambacho mume wake akemkifwata humo ndani.
“Unafanyaje baby?”
“Ngoja”
Raisi Praygod akaminya batani nyekundu iliyomo katikati ya chumba hicho, hapo ndipo kuta zote za chumba hicho zikafunguka, Rahab hakuamini baada ya kukutana na silaha nyingi ambazo baadhi anazifahamu kutokana na mafunzo aliyo weza kuyapita kipindi cha nyuma akiwa na wezake ambao hadi sasa hivi hatambui ni wapi walipo.
“Waoooooo………!!!!”
Rahab alishangaa sana, akataka kugusa bunduki moja ila raisi Praygod Makuya akamzuia asiiguse
“Usiguse, vitu vyote humu ndani zina alama za vidole vyangu, na endapo ukigusa kimoja pasipo mimi kukitoa kwenye sehemu kilipo mlio wa hatari nilazima ulie ndani ya chumba hichi”
Rahab akawa amelielewa hilo, Raisi Praygod akavua nguo na kubakiwa na nguo za ndani, akachukua moja ya suta ya bandi kati ya sura nane zilizomo ndani ya chumba hicho, akaivaa, akamuomba Rahab aweze kumuweka vizuri.
“Inanibidi nifanya hivi”
“Kwa nini?”
“Nchi kwa sasa haipo kwenye usalama na kumbuka ninawindwa na yule mshenzi aliye taka madaraka kwa nguvu amesha toroshwa”
Raisi Praygod alizungumza huku akivaa jaketi la kuzuia risasi, akachukua nguo nyeusi zilizo kwenye moja ya kabati, akazivaa vizuri huku muda wote Rahab, aliendela kumsaidia mume wake pasipo kumuuliza maswali mengi.
“Kama tunakwenda basi vaa bullet proof”
“Halina haja ya mimi kulivaa”
“Kwa nini?”
“Hamna, nisadie bastola moja”
Raisi Praygod akatazama tazama kwenye bastola zake kadhaa anazo zipenda, akachomo moja yenye rangi nyeupe, akamkabidhi mke wake. Wakatoka ndani ya chumba, kila mmoja akiwa tayari kwa safari ya kuelekea kwenye hospitali ya taifa Muhimbili.
“Muheshimiwa hadi mke wako anakwenda?”
Mmoja wa walinzi wakaribu akamuuliza raisi kwa kumnong’oneza kwenye sikoo lake, hii ni baada ya Rahab kuingia kwenye gari alilo andaliwa raisi.
“Ndio”
“Ila muheshimiwa hali ya usalama bado si nzuri”
“Hakuna litakalo tokea”
Mlinzi huyo aliye pewa jukumu la kumlinda raisi hakuwa na kipingamizi cha aina yoyote kwani hiyo ni amri ya kiongozi wake. Safari ikaanza huku gari nne nyeusi, zilizo bandikwa plate number, za kawaidia zikatoka katika geti la ikulu na kuelekea hospitali ya Muhimbili.
                                                                                          ***
“BADO YUPO HAI…………!!!”
Makamu wa raisi aliye weza kumsaliti Raisi Praygod Makuya, alishangaa baada ya kuletewa taarifa kwamba Samson, kijana wake yupo hai.
“Ohooooo sasa itakuwaje, atatoboa siri”
“Ndio hivyo muheshimiwa”
Mlinzi anaye muamini alimjibu kwa usikivu mkubwa sana. Ukimya wa gafla ukatawala ndani ya chumba hichi cha hotel, iliyopo nchini Kenye maeneo ya Malindi. Ukimya huo ukakatishwa na simu ya mlinzi huyo, kwa haraka akaipokea
“Ndio”
“Nimekuelewa”
“Asante”
Majibu ya mlinzi huyo mwenye roho ya kikatili sana, yakaustua moyo wa makamu wa raisi kwani ameamini kwamba taarifa hiyo si nzuri kwa upande wake.
“Raisi Praygod Makuya anaelekea hospitalini kuonana na Samson”
“WHAT………!!!”   

Makamu wa raisi alijikuta akiishiwa na nguvu, akajibwaga kwenye sofa lililopo karibu yake akibaki amemtumbulia mimacho mlinzi wake huyo.

==> ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Sponsor