Advertisement

Breaking

Thursday, September 15, 2016

Majambazi 10 yateka magari, yaua dereva

Wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani wamevamiwa na majambazi yapatayo 10 ambayo na kumuua kwa risasi dereva aliyegoma kuwapa fedha na simu.

Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema wafanyabiashara hao walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe yamepangwa barabarani kuzuia magari.

Amesema baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo majambazi hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu walipoibuka na kufyatua risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara hao wasalimishe fedha na simu zao za mkononi.

No comments:

Post a Comment

Sponsor