Advertisement

Breaking

Sunday, September 25, 2016

Pastor Myamba: Waigizaji ndio wanaua soko la filamu


Muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Emmanuel Myamba maarufu kwa jina la Pastor Myamba ameitaja sababu ya kushuka kwa soko la filamu nchini kuwa ni kutokana na wasanii wenyewe.

Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha Ulimwengu wa Filamu cha TBC 1 kuwa wasanii wamekuwa wakipunguza juhudi za kutengeneza sinema nzuri kwa ajili ya kupunguza gharama.

“Kama watu hatutajiami na kazi zetu tutakuwa ni waajabu. Kuna changamoto ambazo zipo lazima kama wasanii tuzikubali kweli tumefeli. Kwanza kabisa kutengeneza sinema zisizokuwa na nguvu, sasa hivi watu wengi hawapendi kutengeneza sinema zenye nguvu kwa sababu soko limeshuka,” amesema Myamba.

“Tunapunguza juhudi ili tusitumie hela nyingi. Lakini ukweli ni kwamba pale soko linaposhuka juhudi lazima ziongezeke kuweza kuliinua,” ameongeza.

Kwa sasa muigizaji huyo anamiliki chuo cha sanaa cha TFTC ambacho alikianzisha mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment

Sponsor