Advertisement

Breaking

Sunday, September 11, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 1 & 2

Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA

 Mioyo ya watu wengi wanao jishuhulisha nje ya eneo hili la Benki hii ya kijamii baada ya kundi la wasichana wapatao watano wakiwa na  bunduki zenye uwezo mkubwa wakiwa na kazi moja iliyo wapeleka katika eneo hili ambayo si nyingine zaidi ya kushambulia askari yoyote atakaye jipendekeza katika shuhuli ya uibaji wao wa fedha ambao wameidhamiria kwa siku nyingi na leo ndio hitimisho la mipango yao.Wamejitolea kufa na kupona huku kila mmoja akiwa makini sana na upigaji wake wa risasi zinazo toka kweye unduki zao za kila aina.

Wasichana wawili wakaingia ndani na mkuwalaza chini wahudumu wote wa benki pamoja na wateja ambao wapo ndani ya benk hii na hawakuwa na huruma kwa yoyote aliye inyanyua shingo yake kwa madai ya kuwatazama ni kina nani ambao wanafanya kazi hiyo na ambaye alijaribu kufanya hiyo basi risasi kadhaa kama si mbili basi ni zaidi ya mbili zinatua kwenye mwili wake

Wakamkamata meneja wa benki na kumuamrisha awapekeke kwenye chumba cha kuhifadhia pesa hizo na bwana Turma hakuwa na ubishi zaidi ya kuongoza hadi kwenye chumba wanacho hifadhia pesa pamoja na vito vya dhamani kama madini ya kila aina yenye dhamani kubwa sana katika mauzo yake.


Agnes akashusha mabegi makubwa matatu chini alilokuwa ameyabeba mgongoni na akayafungua na akaanza kazi ya kuviingiza vibunda vya pesa pamoja na vipande vya madini,begi lakwanza likajaa na akahamia kwenye begi jengine na kazi ikawa ndio hiyo hiyo ya kuweka pesa kwenye mabegi hadi mawili yakajaa babisa na jengine likafika nusu
“Anna take it”(ana chukua hilo)


Agnes akamsukumia Anna begi moja ambaye kwa wakati wote alikuwa amaishika bunduki yake kiumakini na kuielekezea kwa bwana Turma.Wakati ndani yakiendelea Alima,Rahab na Fety kazi yao ikwa nikuhakikisha hakuna kiumbe yoyote ambaye anaweza kujipenyeza na kufika katika eneo la nje ya banki.Gari tatu za watu binafi zilizo kuwa zinajaribu kukatisha katika eneo la karibu yao wakijifanya ni vichwa ngumu hawaelewi ni kitu gani kinacho endelea walizishambulia kwa risasi nyingi na kuwaua madereva pamoja na watu walimo ndani ya gari hizo
“R nenda kacheki ndani waambie waache pozi hapa nje hali ishakuwa tete”


    Fety alizungumza huku sura yake akiwa ameiziba na kofia maalumu ambalo limetobolewa sehemu za macho tuu na kofia lake linafanana na wezake wote waliomo ndani huku wakiwa wamevalia majaketi maalumu ya kuzuia risasi kupenya(bullet proof) huku suruali zao zikiwa ni nyeusi zenye mifuko mingi pamoja  na viatu vyeusi vya jeshi.


Rahab akaingia na kumuona askari mmoja akijaribu kunyata akielekea kwenye chumba cha kuhifadhia pesa huku akiwa na bunduki mkononi,Rahab hakufanya masihara zaidi ya kufyatua risasi zipatazo tato zilizo ukatisha uhai wa askari huyo na kumuangusha sakafuni kama mzigo na watu wengine wakavifunika vichwa vyao huku baadhi yao wakishindwa kuzizuia haja zao ndogo

Ikamlazimu Anna kuchungulia baada ya kusikia milio ya bunduki na kumuona Rahab akiwa anamgeuza geuza askari ailiye mpiga risasi kwa kutumia mguu kuhakikisha kama amefariki dunia au laa.


“Oya best fanyeni fasta tuibuke zetu hao machalii huko nje wamesha aanza kubweka kama bweha si munajua tena”
“Ndio tumemaliza njoo unyanyue hii ishu hapa”
Rahab akaingia na kuchukua begi lenye pesa nusu na kuliweka mgongoni na wakatoka wakiwa wameongozana huku kila mmoja akiwa ameishika bunduki yake vizuri
“Simameni juu wote”


Rahab alizungumza na kuwafanya wezake kushtuka
“Wewe unataka kufanya ishu gani tena twende zetu”
“Ngojeni musiwe na papara wanangu huko nje kimesha nuka na tukitoka hivi hatuwezi kufika mbali”


Wakamuacha Rahab afanye anacho taka kukifanya,Rahab akawaamrisha watu wote kuvua nguo zao hakujali kama kuna mkubwa au mdogo,msichana au mvulana wote jukumu lilikwa ni moja.Watu wote wakavua nguo zao zote na kubakiwa kama walivyo zaliwa na wote akawaamuru kufungua milango ya benki na kutoka nje na kukimbia la sivyo wote atawachakaza kwa risasi.


Alima na Fety wakashangaa kuona kundi kubwa la watu wakitoka wakiwa wapo uchi wakikimbia,Rahab,Anna na Agnes wakatoka wakijichanganya kwenye watu hao na Rahab akamrushia begi Fety na akaanza kuwashambulia askari ambao ndio wanasimamisha gari lao ili wapambane nao.

Rahab akaendelea kuwashambulia askari wapatao wanne na kuwafanya wapoteze maisha na wezake tayari walisha ingia ndani ya gari lao aina ya Rage rover,Idadi kubwa ya watu waliomo kwenye eneo hili wakaanza kutawanyika kila mmoja kuyanusuru maisha yake na kama mtu alihisi kama hayapendi maisha yake basi alijikuta akijerushiwa na wasichana hawa wenye roho za kikatili huku wakirusha mabomu ya machozi yapatayo kumi yaliyosababisha moshi mwingi katika eneo hili na watu wengi wakajikuta wakitokwa na machozi pasipo kupenda 

Rahab akatupa bunduki yake na kuichomoa bastola yake na kujichanganya kwenye watu wanao kimbia kimbia wakiwa wamechanganyikiwa huku wezake wakiwasha gari lao na kutokomea wasipo pajua.


Dickson fundi maarufu wa baiskel eneo la benki ya biashara iliyo vamiwa na majambazi,naye akawa ni miongoni mwa watu walio jilaza ndani ya kiduka chake huku wakisubiria heka haka za majambazi kutoweka isitoshe moshi wa mabomu ya machozi ukiwaadhiri sana.Akastukia msichana akiingia ndani ya kiduka chake cha na kumuomba hifadhi ya muda,Dickson hakuweza kubisha kutokana na msichana huyo kushika bastola mkononi na kwa haraka akatambua ni miongoni mwa wale majambazi walio ivamia benki

“Ingia humo ndani”
Dickson akamuongoza Rahab kuingia ndani ya kijichumba anacho hifadhia spea mpya za baiskeli anazo ziagizia kutoka Zanzibar.
“Kaka ninakuomba usiseme chochote kwa mtu yoyote sawa”
“Sawa nimekuelewa”


Katika siku ambayo Polisi wanapata shida sana ni siku hii ambayo Benki ya CNB kuvamiwa na majambazi na kushindwa kumkamata jambazi hata mmoja na isitoshe wananchi wamedhalilishwa kwa kutembezwa uchi .Msako mkali ukaanza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam na kila gari zinazo kwenda mikoani ni lazima zikaguliwe na kitu ambacho kinawaumiza akili askari ni kutoweza kuwafahamu majambazi hao japo kila wanapo wahoji hoji wahanga wa tukio hilo akiwemo meneja wa Benk ambaye muda wote analia kama mtoto mdogo anadai kuwa majambazi hao ni wasichana tena wanao onekana kuwa na umri wa miaka kati ya 21 hadi 25


“Huko nje vipi polisi wapo bado?”
Rahab alimuuliza Dikson ambaye anakazi ya kuchungulia nje kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea
“Ndio wapo wanatoa toa maiti za watu walio kufa na kuweka mikanda ile ya njano”
“Ahaa powa”


Rahab akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine na kubakiwa na boxer na kumfanya Dikson kumshangaa jinsi uzuri wa Rahab ulivyo kwani ni mrefu kiasi,sura yake ndogo iliyo jengwa na macho malaini na mazuri ya kuvutia,pua ndogo iliyo chongoka kidogo na unaweza kusema ni jamii ya mabinti warembo wa kisomali,Wembamba wake unavigezo vya kumfanya kuwa miongoni mwa wasichana wanao stahili kugombania umisi Tanzania hata umisi wa Dunia.


Rangi yake ya mwili ya kahawia inazidi kuufanya mwili wake kuwa kivutio kizuri mbele ya macho ya Dikson na kumfanya abaki akiwa amemtizama kwa dakika kadhaa gafla akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola iliyo shikwa na Rahab
“Usishangae sana kijana”


Rahab alizungumza huku akiishusha bastola yeke chini na kumafanya Dickson kuirudiasha sura yake kwenye tukio la askari wanaondelea kufanya mahojiano na watu walio kuwepo katika eneo hili.Dickson akamshuhudia bodo boda mmoja wa pikipiki akizungumza na askari wawili ambao akanyoosha kidole chake kilipo kiduka chake akiashiria kuna kitu wakakitazame ndani ya kiduka hiki na taratibu askari wakaanza kupiga hatua za kuelekea kwenye kaduka ka Dikson


“Shiiti polisi wanakuja huku”
“Wapo wangapi?”
“Wawili”
“Wameshika bunduki mkononi”
“Sasa wewe jikaushe na atakaye ingia humu ndani halali yangu”
“Mmm”
Tayari polisi wamesha fika nje ya duka la Dickson na kuanza kulitazama tazama kwa umakini


                                         ****


Fety anaendelea kukanyaga mafuta ya gari lao akizidi kuliacha jiji la Dar es Salaam na kuutafuta mji wa bagamoyo na ndani ya dakika ishirini wanaingia kwenye mmoja wa msitu  mnene ambao mara nyingi watu hawautembelei na wakalisimamisha kwenye kibanda kimoja kidogo na wakashuka ndani ya gari na Agnes akafungua mfuniko wa chuma ulio jengewa chini ambapo ndipo ilipo kambi yao ya maficho.Kila mmoja akili yake ikawa na kazi ya kumuwazia Rahab ambaye wamemuacha jijini Dar es Salaam
“Jamani kwa mfano R akakamatwa hamuoni kama itakuwa ni shida kubwa sana kwentu?”


Fety alizungumza huku akiliweka chini begi lililo jaa pesa na madini
“Mimi mwenyewe ninogopa asije akatutaja na kila kitu kikaingia dosari”
“Sasa tutafanyaje kwa maana kama ni simu tuliziacha huku na hapa hatuna mawasiliano naye”
“Masikini R wetu cha msingi tumuombee kwa Mungu isiwe kama tunayo fikiria”


Anna akapiga hatua hadi kwenye Tv kubwa iliyopo kwenye handaki lao na kuiwasha na kuanza kutafuta chanel yoyote ya Tanzania ambayo inaonyesha tukio la uvamizi wao.Akafanikiwa  kuiona taarifa ya habari inayorushwa na kituo cha taifa TBC 1 na wote wakakaa kimya huku macho yao na masikio vikiwa vimeelekea kwenye Tv hiyo.


{HADI SASA MAJAMBAZI HAO HAWAJULIKANI NI WAPI WALIPO ILA KWA MUJIBU WA KAMANDA MKUU WA POLISI BWANA IZAK KIMARIO AMEKIRI KWAMBA MAJAMBAZI HAO WALITUMIA BUNDUKI ZA KIVITA NA PIA WAMEWAUA WATU NANE AKIWEMO POLISI MMOJA}
(“Tutahakikisha majambazi hao tunawatia nguvuni kwa maana hili ni tukio ninaliita ni tukio la kigaidi ambalo sisi kama jeshi la polisi hatuta lifumbia macho hata kidogo)


Anna akazima Tv na kuwageukia wezake ambao kila mmtu amekaa kwenye mkao wake  wa kufikiria nini cha kufanya.
“Jamani cha msingi nikuweza kuwasiliana na Dokta Wiliam aje atufanyia upasiaji wa hizi sura za bandia alizo tuvisha”
“Hilo ndio la msingi inatubidi tusitoke nje hadi uweze kufanyiwa upasuaji wa sura zetu”


Agnes akakubaliana na wezake na ajachukua jukumu la kumpigia Dokta Wiliam kutoka nchini Israel na wakampa taarifa juu ya kazi wanayo hitaji kufwanyiwa.Wakakubalina na dokta Wiliam aweze kutuaTanzania na uzuri ni kwamba dokta Wiliam anapafahamu kwenye makazi yao.


Wakiwa wamo ndani ya handaki lao gafla mlio wa hatari ukaanza kulia kwenye moja ya king’ora walicho kiweka kwenye kona ya handaki lao,Kwa haraka Halima akanyanyuka na kusimama kwenye meza yenye kompyuta zipatazo nne na akaziwasha na kuona askari wengi wakiwa na mbwa wakishuka kwenye magari yao mwanzo wa msitu.Picha za video za askari wanao ingia kwenye msitu huu zinaonyeshwa na kamera za ulinzi walizo zifunga kwenye miti umbali mkubwa kutoka katika sehemu lilipo handaki lao.


Wakakumbatiana kwa pamoja huku machozi yakiwamwagika kwa uchungu kwani siku ya leo wanahisi wanaandika historia nyingine mpya tofauti na walizo wahi kuzipitia huko nyuma.
“Sisi ni familia moja endapo itatokea tukafariki basi ninaamini tutakwenda kuonana mbinguni”


Agnes alizungumza huku akijikaza katika kuzungumza kisha kila mmoja akambusu mwenzake kwenye paji la uso na wakaokota bunduki zao na mabegi ya pesa wakaficha kwenye moja ya chumba na kutoka nje ya handaki wakiwa wamejiandaa tayari kwa mapambabo ya kufa na kupona


                                        ****


Ni kikundi kidogo cha watoto wa kike wa mitaani wenye umri isiyo pishana sana kiasi kwamba wanajikuta kutengeneza ushirikiano wao kwenye kuanza kuzitafuta kazi ili kuweza kuyasongesha maisha yao mbele.Hawa si wengine bali ni Agnes,Ana.Alima,Fety na Rahabu ambao wote wazazi wao wamefariki dunia katika mazingira tofauti tofauti.

Wanakutana kwa mama mmoja kwa jina Maafufu mama Bonge ambaye ana nyumba yake maeneo ya Magomeni na huwatumikisha wasichana wadogo katika kuuza miii yao.Agnes na wezake ni miongoni mwa wafanya biashara wa kuiuza miili yao na pesa zote wanazo zipata wanamkabithi mama Bonge na yeye anawafadhili sehemu ya kulala pamoja na chakula na malipo yao kwa siku ni shilingi elfu moja ambayo haijawatosha katika kununua sabuni za kufulia nguo zao.

“Jamani mimi nimechoka na haya maisha ya unyanyasaji…..Miili tunakwenda kuuza sisi alafu tunamnufaisha mtu mmoja tu”


Anna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga akiwa na wezake katika eneo la kujiuza usiku wa saa nne”
“Anna unadhani yutafanyaje wakati sote hapa mjini hatuna baba wala mama”
“Hata kama jamani,wangapi hawana baba wala mama na wanaishi vizuri tuu na wanakazi nzuri na maisha mazuri sisi kweli tunashindwa kabisa kujitoa kwa lile jimama na kuanza maisha yetu?”


“Unacho kiongea Anna ni kweli mimi pia nimechoka na nilikuwa nikisubiria kupata wezangu ambao wataungana na mimi katika kuachana na hii kazi”
“Jamani anaye ungana na mimi anifwate twende tukachukue nguo zetu kwa lile jimama na tukatafuta pa kuishi”


Anna akajitenga peke yake na wezake wanne ambao ni Alima,Rahab,Fety na Agnes wakamfwata na kuwaacha wasichana wengine ambao kwa madai yao wanamuhofia mama Bonge.Wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwa Mama Bonge na hadi wanafika ilisha timu saa sita kasoro usiku.Wakagonga na Mama Bonge akawafungulia na akaonekana kushanga kuona kundi la wasichana hao wakiwa wamesimama mbele yake
“Nyinyi vipi kazi imewashinda hadi munarudisha vikwato vyenu huku?”


Mama Bonge alizungumza huku akifoka na akastukia Agnes akimsukuma na akawapisha mlangoni na wote wakaingia ndani na kuingia kwenye vyumba wanavyo shindia na kuchukua nguo zao na wakamkuta Mama Bonge akiwa amesimama mlangoni huku akiwa ameufunga kwa funguo huku mkononi akiwa ameshika bastola
“Sasa ole wenu nione mtu anatoa kwato zake hapa pasipo kuwa na sababu ya msingi”


Mama Bonge alizungumza huku bastola yake akiwa amewaelekezea,Rahab akapiga hatua mbili mbele na  kuwaacha wezake nyuma na kumtazama mama Bonge kwa macho makali yaliyojaa hasira,Taratibu wakaanza kumzunguka mama Bonge na wote kwa pamoja wakamvamia na kumuangusha chini huku bastola yake wakiitupa mbali na wakaendelea kumpiga huku wakimziba mdomo mama Bonge.Rahabu akanyanyuka na kuelekea jikoni na akaangaza angaza na kuliokota shoka wanalo litumia kuchanjia kuni na kurudi nalo sebleni


“Nipisheni”   
Wezake wakampisha na kwa kasi ya ajabu akalishusha shoka kwa nguvu na likatua kichwani kwa mama Bonge na kukipasua kichwa cha mama Bonge na ubongo wake ukamwagika chini huku damu nyingi zikisambaa kwenye sakafu


             SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……2

 Wezake wote wakahamaki kila mmoja hakuamini kuona tukio lililopo mbele yao,Rahab akatupa shoka chini na kuwatazama wezake usoni kwa umakini
“Munacho ogopa nyinyi ni nini?”
“Ehee ahaaa hapana” Halima alijibu kwa kubabaika
“Tuutoeni sasa huu mwili”
“Tutaupeleka wapi?”
“Mimi ninaona tukodishe taksi”
“Dereva gani ambaye atakubali kubebea maiti?”
“Sasa itakuwaje?”
Wote wakakaa kimya wakitafakari ni nini cha kufanya,Fetty akawatazama wezake kwa umakini kisha akazungumza kwa sauti ya kujiamini


“Nisikilizeni....Cha msingi ni kumkata kata kama nyama ya bucha kisha tunamuweka kwenye kisafleti na kwenda kumtupa tunapo pajua sisi”
“Mmmmm”
“Agnes usigune unadhani kuna mtu anataka kwenda jela wakati kama huu....mimi bado ninayapenda miasha ya uraiani japo yanachangamoto kama hizi”
“Basi  tuanzeni kuifanya hiyo kazi”


Wakavua nguo zao na kila mmoja akabakiwa na chupi na sidiria na kila mmoja akachukua kitu ambacho anaamini akikata kwenye mwili wa binadamu kitakata,Wakambeba Mama Bonge hadi bafu lililomo ndani ya nyumba na kuanza kumkata kata kiungo kimoja bila huruma
“Angekuwa ngombe huyu mama nahisi saa hizi si chini milioni tungekuwa tumesha pata”


“Anna hembu acha uchizi wako”
“Kweli nawaambia...Huyu mama angekuwa ni ng’ombe ahaa mbona tungepata mshiko wa maana”
“Alafu si ninasikia kuna makabila wanakula nyama za watu?”
“Mmmmm kabila gani hizo?”
“Wapo ila nahisi Tanzania hakuna”
“Tanzania mbona wapo?”
“Kabila gani?”
“Wachawi”


Agnes akaachia msunyo baada ya Fetty kuzungumza pointi isiyo na msingi wowote,Wakaendelea kumkata kata mama Bonge huku wakipiga story za aina mbalimbali hadi wakamaliza kumchangua changua,wakachukua safleti pamoja na vifuko vya nailoni na kuweka viuongo kadhaa kwenye kila kifuko na kuvifunga na vyote kwa pamoja wakavidumbukiza kwenye safleti.


Wakaanza kufanya usafi kila sehemu yenye damu na wakamaliza.Wakaoga kwa pamoja na kuvaa nguo nyingine zilizo watoa tofauti na laiti ukikutana nao barabarani huwezi kujua kama niwauaji
“Jamni safari ya wapi?”
“Kuna mzungu mmoja juzi kati nililala naye yupo maeneo ya mbezi bichi twendeni kwake”


Rahab alizungumza na wote wakakubaliana,wakakodi taksi huku safleti yao wakiingia nayo ndani ya taksi na dereva hakuelewa chochote kinacho endelea.Wakamlipa ujira wake dereva na Rahab akampigia simu dokta William ambaye yupo Tanzania kwa kazi maalumu ya utoaji wa mafunzo ya oparesheni za sura kwa madkatari wa jeshi tu,Dokta Wiliam akaminya kitufe kinacho liruhusu geti la mlangoni kwake kufunguka na Rahab akawa kiongozi wa masafara na wote wakaingia ndani.


“Mmmm Jamani hapa kama ulaya geti linajifungua lenyewe”
“Anna acha ushamba unataka kusema kutembea kuto huko hujaona geti kama hili?”
“Sijawahi”
“Ahee shosti nawe umezidi ushamba”
“Tuachene na hilo je hii safleti niiweke wapi kwa maana nimechoka kuibeba”
“Idumbukize hapo kwenye hayo maua”
Halima akaidumbukiza safleti kwenye maua yaliyo tengenezwa vizuri kisha wakaingia kwenye jumba la dokta Wiliam.


“Ohhh karibuni warembo”
Dokta William alizungumza kwa Kiswahili cha kujing’ata nga’ta na Rahab akamkumbatia Dokta William na kumpiga mabusu ya kinafki kisha wakajibwaga kwenye masofa ya dhamani yaliyomo mule ndani
“Rahab ona wewe leo fanyia mimi Suprize”


“Ndio mpenzi wangu nimekuja kukufanyia Suprize na wezangu ili kama tukikukuta na msichana tumpige sana”
“Mimi wezi saliti wewe kutokana moyo wangu penda sana wewe,shindwa hata fanya kazi kwa mambo yako ya kukatika kitandani fanya mimi Crayz”
Wote wakacheka huku wakimtazama Dokta William
“Usijali kama ni kiuno tuu utakipata leo hadi uimbe wimbo wa Taifa la nchi yako”


“Kweli?”
“Ndio kwani kuna siku ambayo nimeshawahi kukudanganya?”
“Ahhaa utafanya mimi nisirudi nyumbani maana nyinyi Afrika munajoto sana tofauti na wanawake ngozi nyeupe wao baridi sana kama amfibia(viumbe wenye asili ya kuishi kwenye maji)”


“Tuachane kwanza na hilo.....sisi tumekuja kuhamia kabisa hapa kwako na kama unavyo tuona na vibegi vyetu hatuna sehemu sisi ya kwenda wala ya kulala”
“Kuna mashaka jumba lote hili kaa mimi peke yangu tena ona raha kuona sichana rembo kama nyinyi kuja kaa na mimi nitapata burudani kedekede”


“Ni wewe tu ila ninaombi jingine?”
“Ombi gani?”
“Tunaomba gari yako hiyo ya UN twende nayo sehemu mara moja kisha tunarudi?”
“Mbali sana na hapa?”
“Hapana sio mbali kivile na hapa”


“Basi ngoja niwapeleke turudi tufanye sherehee kubwaa”
Rahab akawatazama wezake na wakakubaliana kwa ishara na wote kwa pamoja wakasimama na kuacha vitu vyao,Agens akaichukua safleti yenye mwili wa mama Bonge na wakaingia kwenye gari aina ya pick up Ford na wakamuomba dokta William waelekee nje ya jiji kidogo.


“Sasa hivi saba usiku huko kwenda fanya nini?”
“Kuna mzigo tunakwenda kuutupa”
“Nini tena?”
“Ni mwi......”
“Rahab”
Fety alimzuia Rahabu hakumalizia anacho taka kukizungumza kwa maana kinaweza kikaleta mtafaruku baina yao na mzungu huyu.


“Zigo gani hiyo?”
Dokta William aliuliza huku akiongeza kasi ya gari hadi na kuliacha jiji la Dar es Salaam,
“Ahaa ni mzigo wa kawaida tuu mpenzi wangu wala usijali katika hilo”
“Isije ikawa dawa kulevya”
“Ahaa mpenzi wangu umeona wapi mtu akatupa dawa za kulevya wakati ni dili kabisa hilo”
“Mbona wezako kaa kimya hawapigi story”


“Ahaa wemejichokea kwa maana mama mwenye nyumba wetu leo ametutimua ndio hivyo hatuna pa kwenda”
“Ahaa sasa mimi huku Pwani kuna handaki langu kubwa kama hamtojali nyinyi kaa humo kwa siku kama mbili tatu kisha rudi mjini kwa maana pale nyumbani kwangu kesho fika wakuu wangu toka state of America sasa shindwa nyinyi jui wapi kaa”
“Ehee tena itakuwa vizuri”
“Eti warembo nyinyi mpo tayari kukaa kwenye handaki?”
“Ni wewe tu”


Ndani ya nusu saa gari yao ikaingia kwenye msitu mnene na kutokana na uwezo wa gari haikuweza kukwama kwenye matope yaliyo sababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha asubuhi.Wakasimama kwenye moja ya mti na Dokta William akashuka ndani ya gari na kutembea hatua chake na kufungua mfuniko mmoja wa chuma ambao juu yake kulikuwa  na majani mengi ambayo sio rahisi kwa mtu kuuona mfuniko huo,Akawaita Rahab na wezake na wote wakashuka kwenda chini kwa kutumia ngazi zilizopo kwenye eneo hilo.


Dokta William akawasha taa zenye mwanga mweupe unao kufanya uone kama ni mchana kweupe,Akawasha mashine inayo sambaza hewa ya oksijeni kwenye eneo zima la handaki,Katika handaki lake kuna vyumba nane ambavyo vinne ni vyakulala na vitatu vimehifadhia vifaa vingi ikiwemo bunduki za kivita.


Kila huduma inayo hitajika kwenye nyumba kwenye hili handaki ipo na zimetengenezwa vizuri na kutakufanya ukiishi ndani humo usiwazie kama upo ndani ya pango,Dokta William akawaelekeza jinsi ya matumizi ya badhi  ya vitu ikiwemo jinsi ya kuzitazama kamera za ulinzi zilizo fungwa mbali na eneo la kuingilia hapa msituni kwa kupitia computer zilizomo humu ndani.Dokta William akaondoka alfajiri na mapema kurudi zake Dar es Salaam na ikawa ni nafasi nzuri ya Rahab na wezake kuvizika viungo vya mama Bonge 


                                           *****
Maisha yakazidi kwenda mbele huku kila siku jioni Dokta William akija kuwatembelea Rahab na wezake na kuwafundisha baadhi ya mbinu za kijeshi kwani Dokta William na miongoni mwa wanajeshi wanaotegemewa sana katika jeshi la umoja wa mataifa UN.Kadri siku zinavyo zidi kwenda ndivyo jinsi Rahab,Agnes,Anna,Halima na Fety walivyo zidi kukomaa katika mafunzo ya kijeshi ambayo Dokta William aliamua kuwafundisha ili kuwatumia katika biashara zake haramu anazo zifanya akishirikiana na baadhi ya viongozi serikalini.


“Amini sasa nyinyi kuwa wanajeshi kamili si ndio?”
“Ndio”
“Sasa hapa kuna kazi moja taka nyinyi anza kuifanya kwa umakini na umahiri wa hali ya juu...”
Dokta William alizungumza huku akiwa amesimama kwenye kitambaa cheupe kikubwa huku mwanga mkali unaotoka kwenye kifaa kidogo(projectar) na kuna picha mbili za wanaume zikiwa zinaonekana kwenye kitambaa hicho.


“Hapa kuna watu wawili.....Huyu mmoja anaitwa Karim Yussuf  ni mmiliki wa Sheli za Total kwa hapa Tanzania.....na huyu namba mbili yeye itwa Mansuri ni mfanya biashara wa madini mkoani Arusha na kabla ya kesho kutwa mimi sitaki waona hawa watu kwenye dunia hii”
“Dokta kwahiyo unataka sisi tuwaue hao?”
“Ndio nataka ua huyo Karim sasa hivi yeye yupo Dar kwenye hoteli Serena na huyu Mansuri yeye yupo Tanga hoteli moja itwa Tanga bich resolt”


“Cha kufanya ni nyinyi kwenda kukamilisha hii kazi ndani ya masaa 20 yajayo hawa watu wawe wamefutika kwenye ramani ya dunia”
“Samahani Dokta je hawa watu wana makosa gani hadi sisi tuwaue hilo ni swali namba moja,swali namba mbili je utatuhakikishia vipi usalama wetu na tatu malipo yatakuwaje?”


“Swali zuri Anna...Malipo kila mmoja wenu nitampa milioni kumi shillings na kwakitangulizi nitawapa milioni tano tano kila mmoja,Mbili usalama wenu upo sababu hiyo kazi si yangu ila imetoka ngazi za juu na tatu hata mimi nilipo uliuliza ni kosa gani walilo fanya hawa watu nikaambiwa nikafanye kazi hiyo”
Halima akashusha pumzi nyingi huku akiwatazama wezake ambao wameridhika na kazi hiyo ya mauaji.


“Hakikisheni munafwata kanuni zote za nilizo wafundisha katika mauaji ya kimya kimya kama mutashindwa basi tumieni silaha zozote na hakikisheni mikono yenu munaivalisha gloves ili kuepuka kuacha alama za vidole kwa hao maiti”
“Je na sura zetu tuzaziwekaje?”
“Agnes hapo mutajua ni jinsi gani ya kucheza huo mchezo wa sura zenu na hizi ndizo namba zao za simu”


Dokta William akawatajia namba za simu za watu wanaopaswa kuuawa ndani ya masaa 20.Rahab na Agnes wakapangiwa kwenda Tanga kwenda kumuua Mansuri.Halima,Anna na Fety wakapangiwa kwenda Dar es Salaam kumuua Karimu.Dokta William akawakabidhi gari Rahab aina ya Verosa yenye rangi nyeusi kisha Walio baki akaongozana nao hadi Dar es Salaam huku wote wakiwa amekamilika katika swala zima la silaha.


                                         ******
Kwa mwendo wa masaa manne kutoka mkoa wa Pwani hadi Tanga ukawafanikisha Rahab na Agnes kufika Tanga na moja kwa moja wakaelekea kweneye Hotel ya Tanga beach Resolt na wakachukua chumba kimoja na kuanza kumtafuta Muntar ni wapi alipo.Wakiwa wamejipumzisha pembezoni mwa swimming pool lililopo kwenye hoteli hii wakamuona Muntar akiingia hotelini akiwa ameongozana na wapambe wake wapatao sita wanao mlinda na wanaonekana wapo makini sana kwa kila mtu ambaye anapita karibu na bosi wao.


“Ag mtu mwenyewe ndio yule pale”
“Nimemsoma wangu so tunalianzisha sasa hivi?”
“Hapana tutumie akili nyingi kumuua la sivyo hatuto toka salama humu ndani”
“Una wazo gani kichwani?”
“Uzuri wetu unaweza pia ukampagawisha?”
“Je ni mtu wakupenda wanawake isije tukajipendekeza ikala kwetu”
“Ngoja tuyasome mawazo yake”


Agnes na Rahab wakaanza kumfwatilia Muntar na watu wake kwa kutumia macho ya wizi ambayo wanahakikisha hakuna anaye weza kugundua juu ya swala hilo.Muntar na watu wake wakatafuta sehemu iliyo tulia na kukaa na kuagiza vinywaji.Agnes akasimama na kuishusha suruali yake ya jinzi chini kidogo na kuziachia shanga zake za kiunoni kuonekana vizuri na kwamwendo wa madaha akajipitisha pembeni ya meza ya Muntar na watu wake na kuwafanya watu wa Muntar wabaki wakimkodolea macho ya uchu Ages.


“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzia vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi wake analo lihitaji...


ITAENDELEA....

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia theuniversetz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Sponsor