Advertisement

Breaking

Wednesday, September 21, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 11 & 12

MUANDISHI:EDDAZARIA G.MSULWA
 
ILIPOISHIA....
Anna akamuomba Rahab kuipokea simu hiyo
“Haloo”
“Dokta Will hapa nazungumza”
“Dokta vipi, mbona umetupiga na simu ya mezani?”
“Hilo halina tatizo sana, kikubwa nataka kuwaambi kuweni makini kwani kuna wanajeshi wametumwa kuja kuukagua huo msitu munapo ishi”
“Lini?”
“Unauliza lini? Wanakuja sasa hivi na wapo njia na hii taarifa nimepewa na kiongozi wao”

ENDELEA....
“Sawa nimekupata dokta”
“Cha kufanya ni kufunga handaki na nendeni mbali na lilipo”
“Hapa tulipo, ndio tulikuwa tunatoka, tunakwenda kuv......”
Fetty akamziba mdomo Rahab kabla hajaimalizia sentensi yake
“Mnakwenda wapi?”
“Kununua nguo za kuvaa”
“Sawa”
Rahab akakata simu

“Unajua wewe mtoto ni mwehu” Fetty alizungumza huku amemtolea macho Rahab
“Uwehu wangu upo wapi?”
“Unataka kumwambia kuwa tunataka kwenda kuvamia, hujui mazugumzo yote yanasikiwa kwenye mitandao ya simu”
“Ahaa, nilipitiwa”
“Sio kupitiwa, uacha hilo domo lako kubwa”
“Jamani hebu acheni kurumbana, ehee tuambie kuna ishu gani?”

“Anasema kuwa kuna wanajeshi wanakuja kuukagua huu msitu, na wapo njiani”
“Ahaaaa sasa inakuwaje?” Anna alizungumza
“Dokta amesema tufunge handaki na kuondoka, twende mbali na hapa”
“Mpango umeshakufaa huu” Halima alizungumza
“Sasa, mbona Ni shidaaaa” Agnes alizungumza huku akikaa kwenye kiti

“Jamani, tusiakate tamaa, kikubwa ni kuamua lile tunalo lihitaji” Fetty alizungumza
“Sawa, tunaamua je akili na maarifa yetu yanafikiria kile tunnacho taka kukifanya au tunaamua tuu, mwisho wa siku tufaye madudu ambayo yatatucost kwenye maisha yetu” Agnes alizungumza

“Nyinyi mbona waoga sana, kama maji tumeyavulia nguo tunapaswa kuyaoga” Rahab alizungumza
“Wewe acha misemo yako iliyopitwa na wakati, maji ukiyavulia nguo, ukiona yanazingua si unavaa na kuondoka.Kwani ni lazima kuoga” Anna alizungumza.

“Sikieni,dili limesha kufa kwa maana hapa kila mmoja anazungumza lake.Wapo wanao taka kufanya na wanao kataa.Sasa tuwafikirie hawa nguruwe wanao kuja huku”
 Fetty alizungumza huku akiwatazama wezake, hakuna aliye zungumza zaidi ya kufikiria cha kuzungumza.

“Watu wanasema, mwanaume hakimbii nyumba yake, bali anapambana kuhakikisha analinda mali zake na familia yake.Sisi sasa hivi ni sawa sawa na wanaume.Hapa ndio kwetu, hapa ndio tunapo ishi kwa amani.Hakuna aliyekuwa na kwake zaidi ya kutegemea maisha ya kuliwa na wanaume na kumnufaisha mwehu mmoja” Fetty alizungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo na msimamo

“Tunatakiwa kupambana, tunatakiwa kujilinda, Hatupaswi kukimbia makazi yetu.Kikubwa ni kuanyanyuka na kwenda kupambana na hao wanao jaribu kupambana na sisi.Hatuna uchaguzi mwingine.Simama lady’s”

Fetty alizungumza na kuwaamsha wezake walio kaa,wakazunguka duara moja na mikono yao ya kulia wakaikutanisha pamoja, huku wakiwa wamekunja ngumi.

“Tunatoka watano, tunarudi watano”  Agnes alizungumza
“KWA UMOJA TUNAWEZA”
Walizungumza kwa pamoja, kiasha wakaachiana, Kila mmoja akahakikisha silaha take ipo sawa
“Jamani ninapendekeza, tuvae vinasa sauti kwa ajili ya kuwasiliana kwa pamoja” Agnes alizungumza
“Hapo umenena wangu” 

Anna alizungumza, akafungua kabati ambalo wameweka vinasa sauti, kila mmoja akachukua cha kwake na kukiweka kwenye masikio.Kila mmoja akahakikisha kinasa sauti chake kinafanya kazi

“Mnanisikia?” Halima alizungumza
“Ndio dada Halima” Rahab alijibu
“Fetty si ulivue hili jimwili” Agens alizungumza
“Nitapambana nalo hivyo hivyo”
“Mmmmm, haya big mama”

Wakacheka kwa pamoja na kutoka ndani ya pango,kila mmoja akaende njia yake huku wakiwa wameuzingira msitu wao.Kila mmoja akakaa kwenye nafasi ambayo angeweza kuona uingiaji wa wanajeshi hao waliotumwa kuja kufanya uchunguzi kwenye msitu.Kila mmoja akawa na hamu ya kutumia silaha yake, ambayo ameijaza risasi za kutosha.Masaa yakazidi kukatika pasipo kuona dalili yoyote ya majambazi kutokea kwenye msitu walio kuwepo.

“Jamani, mbona kimya? Agnes aliwauliza kupitia kinasa sauti chake
“Jua ndio linazama hivi” Rahbu alijibu
“Tuvuteni subira, kwa maana inaweza nao wamepanga kuvamia usiku” Fetty alizungumza
“Ahaa, jamani mimi njaa inaniuma” Anna alizungumza
“Wezako tunazungumza la maana wewe unazungumzia njaa hapa” Rahab alijibu

“Kwani kusema njaa, ndio nimekosea jamani?”
“Hujakosea ila ngoja tukamilishe hii kazi kwanza”
“Jamani kila mmoja awe makini kwenye pozi lake tunaumizana masikio” Halima alizungumza
“Powa bwana” Anna alizungumza
Masaa, yakazidi kukatika, hapakuwa na dalili yoyote ya mwanajeshi kutokea katika msitu wao.Hadi inatimu mida ya saa saa tano usiku hali ikaendela kuwa ya ukimya.

”Nimevumilia nimeshindwa, kama ni kuja waje tuu, Mimi ninakwenda kula jamani”
Anna alizungumza huku akisimama
“Hata mimi jamani” Rahab alizungumza
“Wewe si ulisema, tunazungumza ya maana subiri hao jamaa zako”
“Rahab na Anna tuachieni kelele” Agnes alizungumza
“Powa”

Anna akaanza safari ya kurudi lilipo handaki lao, hakuchukua muda sana akafanikiwa kufika kwenye handaki.Mazingira ya handaki akayakuta kama walivyo yaacha.Akafungua mfuniko wa handaki ambao ni wachuma na kushuka chini, huku bunduki yake ikiwa mkononi.Akawasha taa zote na kujirusha kwenye moja ya sofa huku akiwa amejichokea sana, Simu ya mezani ikamstua na taratibu akanyanyuka na kuifwata sehemu ilipo na akaipokea
“Hallo”
“Dokta Wille nazungumza”
 “Eheee”

“Ahaa samahani jamani, ile habari ilichanganywa na haukuwa msitu huo.Nilijaribu kuwatafuta kwenye simu zenu za mikononi na ila hazipatikani”
Anna akajizuia kuliachia tusi ambalo, ni languoni, akaendelea kuushika mkonga wa simu pasipo kuzungumza kitu chochote
“Anna unanisikia?”
“Umemaliza?”
“Samahani jamani”
Anna akairudisha simu sehemu alipo ichomoa, macho yake akayagandisha kwa sekunde kadhaa kwenye simu ya mezani kisha akaachia msunyo mkali

“Oya rudini mlale” Anna alizungumza
“Kuna nini?” Halima aliuliza
“Hakuna jipya, huyo mwehu anasema eti alikosea kutoa taarifa”
Kila mmoja akajikuta akiachia matusi mfululizo na misunyo mingi ya kuonekana kukasirishwa kwa kitendo cha dokta William kutoa taarifa iliyo ya uongo.Wakarudi wote wanne wakiwa wamechoka kiasi kwamba hakua aliye kuwa na hamu ya kuingia jikoni kupika.

“Oya huyu mzee tumfanye nini?” Rahab alizungumza
“Mkaushieni” Halima alizungumza
“Haki ya mama naapa, siku akija akisema, oohh sijui ninakazi, ohaa sijui nini, haki ya mama sifanyi”
 Agnes alizungunza kwa uchungu huku machozi yakimlenga lenga kwa hasira.Fetty akawa na kazi ya kuachia misunyo isiyo na idadi huku akiwa ametizama chini.

“Katika maisha yangu, sipendi kupotezewa muda kabisa”
Halima alizungumza kwa sauti nzito kidogo, iliyo jaa hasira hadi wezake wakamtazama
“Nina hamu na pombe, ninataka ninywe hasira iniishe” Fetty alizungumza
“Twende zetuni town” Anna alizungumza
“Kwani, saa hizi ni saa ngapi?” Rahab alizungumza
“Saa hizi ni saa sita” Anna alijubu
“Tuvaeni basi tuondoke”

Kila mmoja akaingia kwenye chumba chake na kuvaa jinzi iliyo mbana na kwa jinsi walivyo barikiwa maumbo mazuri, mtu huwezi kuamini kama wao ni watu hatari katika swala zima la maangamizi.Kila mmoja alipo hakikisha ametoka chikopa, wakatoka kwenye handaki na kuingia kwenye gari lao huku kila mmoja wao akiwa na bastola yake akiwa ameichomeka kwenye sehemu ambayo anaamini hakuna mtu anayweza kuiona.

Kama kawaida Agnea ndio dereva wao, hadi inatimu saa saba usiku wakawa wamesha fika kwenye ukumbu wa ‘MAISHA CLUB’.Wote kwa pamoja wakashuka kwenye gari huku Fetty akiwa amevalia kofia na kuziachia nywele zake ndefu zikikizunguka kichwa chake na kumfanya sura yake isionekane vuzuri.Wakatafuta meza isiyo na watu na kukaa,wakaagizia vinywaji na taratibu wakaendela kuburudika huku wakiwatazama tazama watu wanao cheza mziki

Uwepo wa kundi la wasichana wapya watano kwenye ukumbi, wenye mvuto sana kupita maelezo, ukaanza kuinua hisia za matamanio kwa mapendeshee waliopo kwenye ukumbi huu.Kila pedeshee mwenye pesa zake hakusita kupeleka ofa ya bia kwenye meza waliyokaa Rahab na wezake.

“Samani dada zangu, yule mzee pale ameniagiza nilete hivi vinywaji”
Muhudumu alizungumza huku akiweka chupa za bia zipatazo kumi,
“Sikia, toa uchafu wako.Mwambie hizo bia anywe yeye, na mimi nimalipia”
Fetty alijibu kwa dharahu huku akitoa nito kumi za elfu kumi na kuziweka kwenye kisahani cha muhudumu

“Fetty wacha bwana tuzipige” Anna alizungumza
“Nyamaza wewe, kwani sisi ni Malaya hadi tulipiwe bia.Wewe kaka hebu ondoka na uchafu wako kabla sijabadilisha maamuzi yakawa mengine”

Muhudumu akaanza kutoa chupa zake, moja baada ya nyingine na akapeleka jibu kwa bwana Turma ambaye ni meneja wa benki ya CNB.Akamwambia jinsi alivyo ambiwa
“Hembu nipe kikaratasi na kalamu” 

Bwana Turma alizungumza, muhudumu akampatia kile ambacho aliomba, wbwana Turma akamkabidhi kikaratasi muhudumu na akamuonyesha ampe dada aliye valia kofia.Muhudumu akamkabidhi Fetty kikaratasi.

“Mizee mingine bwana”
 Fetty alizungumza huku akisunya, akataka kukichana ila Anna akamzuia
“Hembu kisome bwana”
“Atakuwa kaandika ujinga”
“Huwezi jua kilicho andikwa” Agnes alizungumza
“Ahaaaa”

Fetty, akakifungua kikaratasi alicho pewa na muhudumu na kukifungua na kuanza kusoma maandishi yaliyo andikwa
{NAITWA TURMA, MIMI NI MENEJA WA BENK YA CBN, SEMA CHOCHOTE NITAKUPA MTOTO MZURI}
Fetty akawaonyesha wezake kikatasi alicho pewa, na kila aliye kisoma akajikuta akitabasamu

“Fetty tumtekeni” Rahab alizungumza
“Eti eheee”
“Ndio”
“Powa niachieni hiyo kazi”
Fetty alizungumza huku akiupeleka mkono wake kwenye mguu wake wa kushoto ulio vaa kiata kirefu aina ya Travota na taratibu akaanza kuichomoa bastola yake

             SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……12

Anna akaliona tukio la Fetty kuichomoa bastola yake
“Wee Fetty unataka kufanya nini?”
“Hakuna”
“Sio hakuna hebu acha ujinga, hiyo bastola watu wakiiona itakuwa ni shida bwana”
Fetty akairudisha bastola yake kwenye mguu wake, kisha akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia, akawaaga wezake na kuondoka kwa mwendo wa taratibu uliojaa madaha yalio wafanya watu wanaume wengi kumkodolea mimamcho, huku wengine wakianza kuimba wimbo

“Hamsini, hamsini, Mia”
Wakiendana na jinsi makalio ya Fetty yanavyokwenda.Fetty akafika kwenye meza ya bwana Turma na kukaa karibu yake huku sura yake akiwa ameiinamisha chini
“Habari yako mrembo?”
“Salama, tu”

“Mbona unaaibu kiasi hichi,”
“Hapana, sijazoea mazingira haya”
“Ahaa, tunaweza pia kuondoka”
“Tukaenda wapi?”
“Ni wewe tuu,sehemu nzuri ambayo mtoto mzuri kama wewe inaweza ikakufaa”
Bwana Turma alizungumza kwa madoido makubwa, hukua akijitutumua akiamini usiku wa leo utakuwa ni mzuri sana kwenye maisha yake kwa kulala na mtoto mzuri kama huyu

“Popote tu”
“Ahaa basi twende kwenye hotel moja hivi ya kifahari”
Bwana Turma akatoa simu yake kwenye mfuko wa koti la suti yake na kuminya namba fulani na kuiweka sikioni simu yake
“Habari yako Luka”
“Salama tuu”
“Hapo kwako kuna vyumba vizuri”
“Vipo mzee wangu”
“Basi niwekee chumba chenye hadhi ya uhakika”

“Sawa mzee”
Bwana Turma akakata simu
“Tunakwenda Hoteli gani?”
“Inaitwa White Sandas Hotel and Resort, naamini hapo utapapenda, pametulia sana, patakufaa wewe mtoto mzuri”
“Sawa, ngoja niwaage wenzangu”
“Sawa, kwani ni nani zako wale?”
“Ni ndugu zangu”
“Sawa mtoto mzuri”

Fetty akanyanyuka na kwenda walipo wezake, ambao wanaendelea kukata kinywaji kwa kwenda mbele
“Sikieni nyinyi, acheni kunywa, tangulineni kwenye hoteli ya White Sandas Hotel and Resort, Mnapajua?”
“Ndio” Anna akajibu
“Sasa, huyu mzee kaingia kumi na nane zangu cha msingi ni kuwa makini kama ni pombe bebeni mtakunywa baadaye”
“Powa tumekusoma kiongozi” Agnes alizungumza

Fetty akaondoka na kumfwata bwana Rurma alipo, wakatoka nje na kuelekea sehemu ya maegesho ya magari.Bwana Turma akaingia kwenye gari lake aina ya Range rover yenye, nyeusi na inavyoonekana ni mpya.Wakaingia ndani ya gari na dafari ikaanza, huku Fetty akikaa mikao ya hasara hasara kumdatisha Bwana Turma anayemtolea jicho la uchu.

“Hii gari yako umenunua shilingi ngapi?”
“Ahaaa, hii gari nimenunua milioni mia nne hamsini”
“Mbona pesa nyingi, hivyo baby?”
“Ahaa, hizo mbona pesa za madafu.Ninapesa nyingi zaidi ya hizo”

“Ahaaa, ulisema unafanya kazi wapi?”
“Mimi ni meneja wa benki ya CBN”
“Je nikitaka kufungua akaunti, nitaruhusiwa?”
“Kwa swala la akaunti usijali mpenzi wangu, asubuhi nikifika kazini nitakufungulia akaunti yako na kukuingizia milioni hamsini”

“Kweli baby?”
Fetty alizungumza huku akitabasamu
“Ndio mpezi wangu, nitakujengea nyumba kama utahitaji”
“Nitashukuru sana mpenzi wangu”
Kwa kumpagawisha zaidi Bwana Turma, Fetty akampiga busu zito la mdomo bwana Turma
“Baby ninaendesha gari”
Kutokana ni usiku hawakuchukua muda mwingi sana katika kufika hotelini,
“Baby shuka kwenye gari basi”
“Naona aibu, wewe nenda tuu alafu utanijulisha ni chumba gani upo”

“Sawa, nipe namba yako”
Fetty akampa namba ya simu bwana Turma
“Nitakupigia sasa hivi”
Bwana Turma akaondoka hadi kwenye chumba alicho wekewa na Lukas, mkurugenzi msaidizi wa hoteli hii ya kitalii, yenye hadhi ya kitalii.Fetty akatoa simu yake na kumpigia Rahab
“Mupo wapi nyinyi?”
“Sisi ndio tupo Mikocheni sasa hivi” Rahab alizungumza kwa sauti iliyo jaa pombe

“Ahaaa saa zote mlikuwa wapi?”
“Tulikuwa, tunamalizia bia zetu”
“Anaye endesha gari ni nani?”
“Anna”
“Amelewa?”
“Ana unaulizwa na Fetty umelewa?”
Rahab alizungumza huku, akimtazama Anna aliye kaa pembeni yake akiendesha gari

“Hapana”
“Anasema ajalewa”
“Mpe simu nizungumze naye”
Rahab akamuweka simu sikioni Anna
“Anna shosti fanya, mpango mrudi home”
“Kwani vipi?”
“Hao wenzako wamelewa sana, si unajua hali yetu”
“Sawa, ngoja nigeuze gari”
“Nakuomba sana, msirudi club”
“Sawa”

Fetty akakata simu yake, hakukaa sana simu yake ikaita, akapokea na kuisikia sauti ya bwana Turma.Akamuomba aingie chumba namba 27.Akamuelekeza Fetty sehemu ya chumba hicho kilipo na kukata simu,Fetty akashuka kwenye gari na kwenda sehemu alipo elekezwa
                                                                                                 “Anna mbona unageuza gari?”
Rahab aliuliza kwa sauti ya kelele
“Tunarudi home”
“Ahaa, twende bwana”
“Hatuwezi kwenda”
Agnes na Halima wao hawakuwa na usemi wowote, kila kinacho endelea kwao wanaona ni sawa, hii nikutokana na kunywa pombeni nyingi kupita maelezo.

“Kwa nini sasa hatuendi?”
“Rahab umelewa sana, twendeni home tukalale tu”
“Kweli bwana, tukalale”
 Agnes akaunga mkono na kumfanya Rahab kukubaliana na hali halisi.Kwa mwendo wa kasi wa gari yao hawakuchukua muda mwingi sana kufika kwenye handaki lao, kila mmoja akaingia kwenye chumba chake na kulala
                                                                         
Fetty akaingia kwenye chumba ambacho ameelekwezwa, akamkuta bwana Turma amevua nguo zake na kubaki na bukta huku akiwa amejilaza juu ya kitanda.Kwa ukubwa wa tumbo la bwana Turma ukamfanya Fetty kuangua kicheko cha chini chini
“Bab mbona unacheka?”
“Hapana mpenzi wangu, wale wezangu nilizungumza nao wakaniambia kuwa mmoja wao ametapika kwa pombe, hapa ndio ninacheka”
“Ahaa, ni mgeni kwenye pombe?”
“Hapana,ila leo amechanganya pombe”

Fetty alimdanganya bwana Turma ambaye, alisha agizia mzinga wa pombe kali.Fetty taratibu akavua nguo yake ya juu na kubaki na sidiria.Taratibu akakaa kitandani, bwana Turma akaanza kufakamia mipombe mingi akiamini mechi atakayoipiga itakuwa ni motomoto, itakayo mpagawisha Fetty

“Alafu hukuniambia jina lako”
“Ninaitwa Faudhia”
Fetty alimdanganya bwana Turma
“Unafanya kazi gani”
“Mimi nipo tuu nyumbani, wazazi wangu wanakaa Afrika kusini, ila kwa sasa wapo nyumbani likizo”
“Ahaa, wanafanya kazi gani?”
“Wao kule ni madaktari”
Kila anacho kizungumza Fetty ni uongo ulio kubuhu, ila unaendana na ukweli

“Baby benki kwenu mna pesa nyingi eheee?”
Fetty aliuliza kwa sauti ya mitego
“Ndio, tena kesho asubuhi inabidi niwahi ofisini kwani kunapesa nyingi sana inaletwa na wafanya biashara”
“Ni kiasi gani?”
“Ni zaidi ya Bilioni mbili, na ushee hivi”
“Ahaaa, zinaletwa saa ngapi?”
“Mida ya saa moja na nusu watakuwa tayari wameshazileta”
“Ahaaa, ila baby nikuombe kitu?”
“Kitu gani?’

“Mimi, asubuhi naomba niende na gari lako nyumbani kwa maana wazazi wangu ni wakali sana.Wakiniona na gari kama hiyo yako, hata nikiwaambia kuwa ni yarafiki yangu hawata nigombeza sana”
“Ahaaa, sawa.Nitampigia dereva wangu wa kazini aje kunichukua asubuhi”
“Sawa, asante baby”
“Usijali ni vitu vidogo sana kwangu”

Ikawa ni hatua moja aliyoifanya Fetty katika upelelezi wake, Fetty kutokana si mgeni na kazi ya kuuza mwili wake akaanza madoido ya kuzichezea chezea sehemu za siri za bwana Turma na kumfanaya aanze kuweweseka na kutoa vilio vya raha.Kwa jinsi ya utundu wa Fetty katika kuwapagawisha wanaume hususani kama bwana Turma mwenye maumbile madogo ya bunduki zao.Akadumbukiza bunduki ya bwana Turma kwenye mdomo wake na kuanza kuichezea kwa jinsi anavyoweza, bwana Turma akajikuta akipanda mlima Kilimanjaro bila kupenda.
“Baby asante, naomba tulale”

Bwana Turma alizungumza huku akihema kama bata mzinga, Ikawa ni nafuu kwa Fetty, bwana Turma akajigeuza upande wa pili wa kitanda na kulala.Fetty akayatupia macho yake kwenye saa ya ukutani, na kukuta ni saa kumi usiku.Hakuona haja ya kulala zaidi ya kusubiria muda usogee sogee amuamshe bwana Turma.

Saa kumi na mbili alfajiri akamuasha bwana Turma, ambaye amejawa na uchovu mwingi sana na wenge la pombe
“Baby nataka kuwahi nyumbani”
“Nyumbani”
“Ndio, nataka niwahi kabla hata baba na mama hawajaamka”
“Ahaa, hembu niletee hiyo suruali yangu hapo”

Fettya akashuka kitandani na kuichukua suruali ya bwana Turma, iliyoning’inizwa nyuma ya mlango kwenye kijisumari.Bwana Turma akaingiza mkono kwenye surua yake na kutoa kibunda cha pesa, akahesabu noti thelasini na tano za shilingi ellfu kumi kumi, ikiwa ni wasa na shilingi laki tatu na nusu.Akamkabidhi funguo ya gari Fetty
“Baby leo naomba, mida ya jioni urudi tena kwenye hii hoteli sawa”

“Sawa baby, kwani hata mimi sijaridhika”
“Nikitoka kazini nitakuja, tukamuane sana”
Bwana Turma alizungumza huku akipiga miyayo ya uchovu
“Sawa mume wangu”
“Gari hiyo tumia, siku nzima.Kwani mafuta yake ni yakutosha”
“Sawa baby, asante”
“Sawa, na nikija jioni nitakujia na kikadi chako cha benki, nitakufungulia akaunti kwa jina jengine, au wewe unasemaje?”
“Sawa mpenzi wangu”

Fetty akampiga busu bwana Turma na kuvaa nguo zake, kisha akarudia kumpiga busu la mdomo bwana Turma na kuzudi kumchangaya mzee wa watu.
“Yaani kwa ulivyo nifanya jana nipo tayari hata kukuoa wewe mtoto”
“Usijali tutalizungumza vizuri, jioni.Utanikuta humu ndani”
“Sawa nitalipia chumba kwa siku tano”
“Itakuwa vizuri”

Fetty akamuaga bwana Turma na kutoka ndani, moja kwa moja akaelekea sehemu lilipo gari la bwana Turma na kupanda na kuondoka kwa mwendo wa taratibu ili asistukiwe na watu waliopo kwenye hii hoteli.Safari ikaanza huku akiwahi foleni ya magari yanayokwenda mikoani asubuhi.Akafanikiwa kufika kwenye handaki lao, Akawakuta wezake wakiwa wamelala, akaanza kuwagongea mmoja baada ya mwengine

“Jamani, kuna dili la pesa ndefu” Fetty alizungumza
“Ya kiasi gani?”
“Bilioni zaidi ya mbili, pia ni benki tunayo kwenda kuvamia.Sasa ule mpango wa jana tunauhamishia benki hii”
“Benki gani?” Halima aliuliza
“CBN, kila kitu kipo katika mpango.Jamaa jana kanieleza kila kitu, hadi gari ameniachia”

“Wee....!!” Agnes alihamaki
“Ndio, ipo hapo nje”
Wakatoka na kuliona gari la kifahari alilo kuja nalo Fetty.Wakaanza kulikagua huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha sana
“Sasa, kazi ni moja.Pesa pale inapelekwa mida ya saa mbili, sisi tunatakiwa kwenda pale mida ya saa tono, au sita”
“Etii eheee”
“Ndio”

Wakanywa chai ya nguvu kuyapa matumbo yao uhai, wakaanza kujiandaa kila mmoja akahakikisha anachukua silaha yake anayo weza kuitumia, wakachukua mifuko mikubwa, ilio tengenezwa kwa nguo kisha wakaingia kwenye gari na safari ikaanza

“Jamani, umakini ni muhimu sana, kulinda ni kitu kikubwa, Ndani ya benki wataingia wawili, nje watabaki watatu”
Fetty alitoa maelezo yaliyo sikilizwa na kila mmoja.Wakafanikiwa kufika nje ya benki na Fetty akalisimamisha gari kwa kasi na wote kwa pamoja wakashuka kwa haraka, na kuaanza kufyatua risasi hewani, zilizo wachanganya wananchi waliopo kwenye eneo la benki
                                                                                       
 Bwana Turma akafika benki, kwa kutumia gari ya benki moja kwa moja akaingia ofisini kwake na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.Wafanya biashara watatu, wakafika benki kama walivyo weka ahadi yao juzi.Wakakutana na bwana Turma na kuhifadhi kiasi chao kikubwa cha pesa walicho kuja nacho kisha wakaondoka.Fedha zikahifadhiwa kwenye chumba maalumu, ambapo kuna pesa nyingine.Akarudi ofisini kwake, mfanyakazi wake akamuarifu kuna mgeni amekuja kumtembelea.Akaingia kijana aliye valia nguo za kipolisi huku mkononi mwake akiwa ameshika begi, bwana Turma akatabasamu baada ya kumuona kijana huyo akiwa amevalia mavazi ya polisi.

“EDDY, UMEKUWA ASKARI?”
 “HAPANA MJOMBA”
“ILA?”
“AHAA VIJIMAMBO TU,”
“ILA NINASIKIA UNATAFUTWA NA POLISI”
“NDIO, ILA MJOMBA NINAOMBA MSAADA WAKO”
“MSAADA GANI?”
“KUNA HAYA MADINI, YANADHAMANI KUBWA SANA.NINAOMBA NIWAUZIE NYINYI KAMA BENKI NA PESA YANGU MUIWEKE HUMU NDANI, IPO SIKU MUNGU AKIBARIKI, MIMI AU MWANGU ANAWEZA AKASAIDIWA NA HIYO PESA”

Bwana Turma akamtazama Eddy kwa umakini kisha akamuomba Eddy amuonyeshe hayo madini, Eddy akaweka begi juu ya meza na kulifungua na kumfaya bwana Turma kushangaa.

“UMEYATOA WAPI?”
“HII NI MALI YA MAMA, NINAKUOMBA SANA UNIWEKEE”
“WEWE ULIKUWA UNAYAUZA KWA KIASI GANI?”
“BILIONI MOJA NA NUSU SHILINGI”
“MBONA NYINGI SANA”
“HATA HAYA MADINI, YANADHAMANI KUBWA SANA.NIKISEMA NIUZE KWA MASONARA SI CHINI YA BILIONI TANO”
“SAWA MJOMBA NIMEKUELEWA, NGOJA NIKAWAITE WAHASIBU NA WANASHERIA WA BENKI TUWEZ KUFANYA BIASHARA”
“SAWA MJOMBA”    

Bwana Turma akatoka na kwenda kwenye ofisi ya muhasibu, akakubukua kwamba hajamfungulia kipenzi chake akauti kama alivyo muhaidi.Akaanza kumpa maelekezo muhasibu wake juu ya ufunguaji wa akaunti anayo itaka
“Meneje hizo pesa nitoe za benki au zako binafsi?”
“Toa za benki mtu akikuuliza, muambia aje kwangu”
Bwana Turma akiwa anasubiria zoezi la kufungiliwa akauti, gafla milio mingi ya risasi ikaanza kusikika ikitokea nje na kuanza kuwachanganya bwana Turma na muhasibu wake
 
 ITAENDELEA....

No comments:

Post a Comment

Sponsor