Advertisement

Breaking

Tuesday, September 20, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 9 & 10

MUANDISHI:EDDAZARIA 

Ilipoishia...
Dokta Williama aliendelea kuwasikiliza wakuu hawa wa polisi ambao vyeo vyao vinawatambulisha kama ma RPC kwenye mikoa yao.Lifti ikafunguka na wote wakatoka ndani ya lifti.Askari hao wakaendelea kwa mwendo wa kasi na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.Dokta William akajiweka sawa nguo zake na kuingia ndani ya ukumbi huu.Gafla macho yake yakatazamana na midomo ya bastola alizo elekezewa na wakuu wa polisi waliokaa kwenye viti vyao huku wakioneka kukasirishwa sana na uwepo wake

ENDELEA....
IGP bwana Gudluck Nyangoi akwaamuru wezake kuziweka silaha zao chini na wakati
“Karibu dokra Willian”
Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akitabasamu na kumfanya dokta William kushusha pumzi nyingi,kidogo wasiwasi ukaanza kumpungua.

“Jamani huyu ni miongoni mwa wanajeshi wa umoja wa matiafa,yupo hapa nchini kwa ajili ya mafunzo wa madaktari wa jeshi letu juu ya jinsi gani wanaweza kumtengeneza sura bandia”

“Dokta,kwanza samahani kwa kukuvunjia ratiba zako kwa maana haikuwa katika ratiba zako leo kama nitakuitaji hapa”
“Bila samahani mkuu”
“Karibu ukae”

Dokta William akaka kwenye kiti alicho onyeshwa na bwana Nyangoi,akawaytizama makamanda wote waliopo ndani ya ofisi na hapakuwa na hata mmoja anaye mfahamu zaidi ya IGP Gudluck Nyangoi.

“Jamani kama munavyo jua,sisi kama jeshi la polisi tumekubwa na msiba mkubwa sana wakupoteza vijana wetu katika tukio la jana usiku,Pia ni aibu kubwa kwetu sisi kama jeshi la polisi kwa kushindwa kupambana na majambazi ambao,sijajua ni vipi tulishindwa kuwazuia na kusababisha maafa makubwa kama haya”

Ukimya ukatawala,huku akili ya Dokta William ikiwa inajaribu kupanga kitu cha kuzungumza kabla hajaulizwa kwani ametambua umuhimu wake wa yeye kuwa hapa ni kuwashauri viongozi waliopo humu ndani 

“Jamani ninawasililiza,nasubiri maoni yenu.Nini tufanye ili kuwakamata hawa watu na ninavyo sikia wao ni wasichana sasa sijajua inakuwaje wasichana kama hawa wanatushinda kirahisi rahisi?”

“Mkuu mimi ninaona,kwanza tudhibiti mipaka yote ya nchi jirani kwa maana kumbukeni kulikuwa na tishio la kundi la Al-Shabab kuivamia mlimani city.Sasa isije ikwa ndio hao wameanza kutekeleza mipango yao”

“Asante bwana Shaban Mbago,mwengine?”
“Mkuu mimi kuna swala ambalo bado silipatii picha,haiwezekani mpango ule wa kumsafirisha yele binti katika njia ya ardhini ulibumburuka.Swali ni je,ni nani aliye toa siri ile?”

Mapigo ya moyo ya dokta William yakaanza kwenda kasi,ila hakutaka kuiruhusu hali hii kuendelea kuundama moyo wake,akawatazama wakuu wa polisi waliopo eneo hili na kuwaona wengi wapo kimya kila mmoja akikosa cha kuzungumza.Dokta William akanyoosha kidole na bwana G.Nyangoi akampa ruhusa ya kuzungumza
“Wakuu wangu mimi ninajambo moja ninaomba nizungumze”
“Zungumza tuu,kwani ushauri wako ni mkubwa sana”

“Kuna hali ambayo inaendelea ndani ya jeshi lenu,kwa kipindi kifupi nilicho kaa katika nchi hii na kushirikiana na jeshi lenu nikagundua kuna hali amayo sio nzuri na endapo mukiacha ikikua na kukomaa,Siku hadi siku jeshi lenu litazidi kuzalilisha na kuteketea mwisho wa siku ile imani ya kusema kuwa Tanzania ni nchi ya amani itafutika katika vichwa vya watu wengi”

“Viongozi kwa viongozi hamuaminiani,hilo ni la kwanza.Pili viongozi mumekuwa ni watu wakuunda vikundi vikundi vya watu ambao munawatumia kwa maslai yenu binafsi na si ya taifa.Kwa mfano kuna magaidi ambao jeshi la polisi mulikuwa munawatafuta kwa kipindi kirefu sana.

Kutokana na uaminifu finyu wa baadhi ya viongozi magaidi wale wakaendelea kudumu na kuishi kwa kipindi kirefu pasipo serikali kuzungumza kitu cha aina yoyote.Kila mulipo kuwa munajaribu kwenda kuwakama walikuwa wanawakwepa na kubaki mukijiuliza mutafanya nini?”

“Kabla ya hichi kikao kuendelea,jiulizeni je hakuna wasaliti watako vujisha siri juu ya watu muna watafuta? Na kama wapo je kuna haja gani ya hichi kikao kuendelea kuwepo hapa?”

Ukumbi mzima ukakaa kimya,sura za makamanda wote wapolisi zikawa zikimtazama Dokta William ambaye amezungumza maneno ambayo wengi wao hawakuwa wanayafikiria kuyazungumza

“Musikalie kuunda tume kuchunguza vitu ambavyo munajua majibu yake kabla ya kuzungumza.Nyinyi ni jeshi,munatakiwa kuwa kitu kimoja na si kuwa katika mgawanyiko ambao utawakost garama ambazo si za msingi.Jaribuni kuiga baadhi ya mbinu za kijeshi katika mataifa makubwa yaliyo endelea,mfano Marekani na kadhalika.Nitatolea mfano mdogo tuu wa wa wale wanejeshi walio tumwa kwenda kumuua Osama Bin Laden,Gaidi ambaye sisi kama Israel alituumiza pia vichwa jinsi ya kumpata”

“Ila kikosi cha wanajeshi wachache walio tumwa kuumuua Osama,kilikuwa ni cha siri kubwa hata makamu wa raisi wa Marekani hakuwa analifahamu hilo,zidi ya raisi Obama na wasadizi wake,Na tukio zima lilipokuwa linaendelea walikaa kwenye chumba maalumu pasipo na mtu yoyote kuwa na mawasiliano ya simu ya mkononi,hata raisi mwenyewe alizuiwa kuwa na simu.

Huo ni mfano mdogo ila hapa hapa ninashanga muheshimiwa unaendeleza kikao ila kuna huyo bwana hapo anachati na simu chini ya meza,Je kuna umuhimu gani wa hichi kikao?”
Bwana Noel Muro akastuka na kuuingiza simu yake mfukoni baada ya kunyooshewa kidole na Dokta William.
“Muro ninaomba uzime simu yako”

Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akimtazama bwana Muro
“Mkuu cha mwisho kukizungumza ninawaomba,muunde kikosi maaalumu cha siri kitakacho wa pambana na hili swala.Asanteni”
Dokta William akakaa kwenye kiti na viongozi wote wakampigia makofi wakimpongeza kwa ushauri wake alio utoa.

“Dokta Willim asante sana kwa ushauri wako mzuri sana.Mimi ningekuomba usaidiane na mimi kuunda kikosi kitakacho weza kuwasaka hawa majambazi.Nipo radhi kuwaishawishi serikali kuongezea mshahara”
Laiti IGP bwana G.Nyangoi angegundua mtu anaye muomba juu ya huo mpango ndio muhusika nambari moja wala asinge zungumza hayo maneno

                                             ***

Kutokana na uelewa mkubwa wa Agnes katika maswala ya usomaji wa ramani akaanza kuwaelekeza wezake jinsi ya kuingia katika benki kuu ya taifa BOT kufanya tukio wanalo taka kwenda kulifanya.Maelekezo yake hayakuwa magumu sana kwa wezake kuyaelewa,Kila mmoja alielewa vizuri na palipokuwa na swali wakawekana sawa
“Ag tumesha isoma ramani nzima je,jinsi ya kuingi hapo itakuwa vipi?” Anna aliuliza

“Hapa kikubwa cha kufanya ni kuvaa miili ya bandia”
“Kivipi tutavaa miili ya bandia?”
“Sio sote tutavaa miili ya bandi,ila kati yetu mmoja atavaa mwili ambao utamfanya aonekane kama bibi kizee,atakwenda ndani ya benki huku katika kifungo cha ngoo yake kuna kamera ndogo ambayo tutaifunga na jinsi anavyo kwenda sisi huku nyuma kupitia simu zetu tutaweza kuona jinsi madhari ya ndani na jinsi ulinzi ulivyo”
“Agnes naamini leo tutakuchosha na maswali mengi,je hiyo kamera itakuwaje kuwaje?” Rahab aliiuliza

“Ngoja nimsaidie kujibu,Kamera ambayo itatumika ni ndogo sana na ipo kama jicho fulani hivi ambako tunaweza kulibandika kwenye kifugo cha nguo pasipo mtu yoyote kujua”
Fetty alimjibu Rahab
“Kamera na mwili huo vitapatikana wapi?”
“Kuna muarabu mmoja pale kariakoo anauza hivi vitu  ila ni kwa siri sana,Japo duka lake linauza urembo wa vitu vya kupambia nyumba” Agnes alizungumza

“So ni nani atakwenda kununu?”
Wakaa kimya huku kila mmoja akiwa kimya.
“Mimi nitakwenda?” Halima alizungumza na kuwafanya wezake kumtazama
“Sawa,itabidi tukafanyie make up itakayo kubadilisha hata muonekano wako”  Anna alizungumza
“Mimi nitakufanyia make up” Rahabu alizungumza 

“Ok kazi inafanyika lini?” Agnes alizungumza
“Kazi ya kununu vitu inaanza leo”
“Je siku ya kwenda kupiga tukio ni lini?” Halima aliuliza
“Hata kesho ikiwezekana kikubwa ni kuwa makini na lile ambalo tunalifanya”
“Mmmm,tuacheni hali huko nje itulie”
“Tukiwaacha wakijipanga itatuwia vigumu.Kikubwa ni kupiga tukio litakao waliza miaka yote” Fetty alizungumza huku akiwatazama wezake

Wakaanza kazi ya kumfanyia ‘make up’ Halima,wakamvalisha wigi la nywele lilo mbadilisha muonekano wake na kuzidi kuwa mzuri zadi,wakamuweka nyusi bandia zilizo zidi kumpendezesha.Hadi wanamaliza Halima akawa tofauti sana na jinsi alivyo,akavalia suruali iliyo mbana makalio yake ya wastani na kuziachia hipsi zake kuonekana vizuri

“Haki ya nani,ningekuwa mwanaume Halima ningekutongoza”
Rahab alizungumza na kuwafanya wezake kucheka
“Kweli vile,cheki mtoto alivyo bomba.Unaweza kusema ameshushwa kutoka mbinguni kumbe kwa shabaha za bunduki ni mwengine kabisa”
“Hembu Rahab acha ujinga bwana”

“Sasa hivi ni saa tano asubuhi,tukikusindikiza hadi pale barabarani itatuchukua kama dakika ishirini si ndioa?” Fetty alizungumza
“Ndio”
“Oya shosti kama kuna uwezekano utujie na gari basi”
“Gari bila hela litatokea wapi,Mbinguni?”
“Ahaaa tuchangeni changeni hata kaVitz kamilioni tano” Rahab alizungumza
“Ok kila mmoja atoe Milioni moja”

Wakakubaliana kila mmoja akatoa milioni moja moja na kumkabidhi Anna,Safari ya kumsindikiza mwenzao ikaanza huku njia nzima wakiwa wanazungumza na kila mmoja akiwa na bastola yake kiunoni.Njia nzima wakawa na kazi yakusimuliana stori zisizo na kichwa wala migu,wakafanikiwa kufika barabarani na wao hawakutoka kabisa barabarani na kumuacha Anna asimame mwenyewe barabarani huku akiwa na pochi ndogo aliyo ining’iniza kwenye kwapa lake

Anna akaisimamisha gari ndogo,kwa bahati nzuri gari ikasimama,akapiga hatua za haraka hadi sehemu ilipo simama na kuzunguka upende wa dereva na kuwakuta vijana wawili
“Samahani kaka zangu?”
“Bila samahani mrembo?”
“Ninaombeni lifti mimi ninakwenda Dar es Salaam”
“Ingia twende kwani na sisi tunakwenda Dar”

Anna akaingia siti ya nyuma na gari ikaondoka,Rahab na wezake wakarudi kwenye handaki.Anna akamtumi wezake meseji
(JAMANI HAWA WAKAKA WANAVUTIA)
(Umeshaa anza,jua kilicho kupeleka achana na hizo habari) Halima akawa wa kwanza kuijibu meseji
“Sister unaitwa nani?” Jama mmoja aliye kaa pembeni ya dereva alizungumza

“Mimi ninaitwa,Hilda” Anna alidanganya
“Ahaa mimi ninaitwa Jackson na huyu kaka yangu anaitwa John”
“Nashukuru kuwafahamu”
“Wewe unafanya kazi gani?”
“Mimi ni mke wa mtuu,najaa nyumbani kwa mume wangu”
“Ahaa,daa kweli wewe ni mke wa mtu kwa maana unavutia sana”

“Asante”
“Sisi bwana ni waanya biashara wa madini,Tunatokea mererani”
“Ahaa hongereni”
“Sasa sijui leo tunaweza kuwa pamoja”
“Ahaa mume wangu bwana ana wivu sana”
“Ahaaa,kawaida mbona.Kila mmoja na chake”

Wakaendelea kuzungumza hadi wanafika maeneo ya Mbezi wakakuta msururu mrefu wa magari,Anna akastuka baada ya kuona askari wengi wakiwa wanakagua gari mmoja baada ya jengine.Askari wawili wafika wenye gari alipo Anna na kuwaomba wote watatu kushuka ndani ya gari jambo lililo anza kumuogopesha askari mmoja akawa amemkazi macho sana Anna akionekana kumtilia mashaka......

            SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……10

......Redio za upepo za polisi zikaanza kusikika zikiokoroma na sauti kali ikasikika
“Kunaajali ya moto huku kwenye magari ya mbele,Over”
“Tunakuja.Over”

Askari mmoja alijibu na kuwaacha Anna,John na Jackson wakirudi ndani ya gari.Wakisubiria foleni iweze kusogea.
“Hivi jamaa alisema kuwa kuna moto mbele” John aliuliza baada ya kuona watu wengi wakikimbilia mbele
“Hembu,ngoja”
Jackson akashuka ndani ya gari na kukimbilia mbele,akakuta gari moja ndogo aina ya Subaru ikiwaka moto na wananchi wakijitahidi kuzima gari hiyo.Jackson akarudi kwenye gari

“Kuna gari hapo mbele inateketea”
“Ipo kwenye foleni” Anna aliuliza
“Ndio Hilda”
“Hakuna aliye jeruhiwa”
“Sidhani kwa maana hakuna mtu yoyote ndani ya gari”
Hali ya foleni ikazidi kuongezaka na kusababisha msongamano mkubwa wa magari
“Napoteza muda tuu”

Anna alijiseme kimoyo moyo huku akitazama nyuma kuyaangalia mabasi mengi yanayo tokea mkoani yakiwa yemejipanga kwa wingi yakisubiria gari za mbele kusogea.
“Jamani ngoja nikanunue maji pale dukani”
“Lete pesa yako nikakununulie,maji” Jackson alizungumza
“Hapana wee acha tuu nitanunua tu hapo juu”

Anna akashuka kwenye gari na kuvuka upande wa pili wa barabara huku akiwa makini asiweze kugundulika kirahisi, kwa kuzuga akaingia kwenye duka moja na kuagiza maji makubwa ya chupa, akiwa anasubiria kukabidhiwa maji na muuzaji akastuka baada ya kuona picha ya Fetty ikitangazwa kwenye taarifa ya habari kwenye kituo cha ITV

(JAMBAZI HUYU, NA WENGINE BADO WANAENDELEA KUTAFUTWA NA JESHI LA POLISI.KIKOSI MAALUMU.UKIMUONA SEHEMU YOYOTE TUNAKUOMBA UWASILIANE NA JESHI LA POLISI KUPITIA NAMBA YA SIMU +225 657072588)

Muandishi wa habari alizungumza na kumfanya Anna kubaki akitazama chini, akakabidhiwa maji na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kuondoka kabla hajapia hatua hata tano akastukia akiitwa na sauti ya kiume nyuma
“Dada umesahau chenchi yako”

Jamaa mmoja, aliye simama kando ya duka alimuambia Anna ambaye anatumia jina la bandia la Hilda.Anna akarudi haraka haraka hadi dukani na kuichukua.Akawatazama Jackson na John ndani ya gari na kuwaona wamejilaza kwenye siti zao huku kila mmoja akiwa amejochokea kiasi kwamba anatamani gari lake liruke hadi mbele kusipo kuwa a foleni na kuendelea na safari zake.

Anna akaanza kutembea kuelekea mbele kulipo tokea janga la moto huku macho yake yakiwa makini sana na polisi wanao wazudia watu kuisogelea sehemu ambayo gari linaungua na kuwaacha askari wa zima moto kufanya kazi hiyo.Akafanikiwa kupita pembezoni mwa barabara hadi sehemu walipo waendesha pikipiki(bodaboda)

“Kaka hapa hadi kariakoo ni bei gani?”
“Ahaaaa dada hapo kwa kumi natano”(elfu kumi na tano)
“Powa twende”
Anna akapanda kwenye pikipiki
“Naomba Helmet”
Akapewa Helment na kulivaa, safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya.
“Kaka usipeleke kasi sana,nyinyi waendesha pikipiki siwamini”

“Kwa nini hutuamini?”
“Ahaaa nyinyi bwana pikipiki munajifunza leo kesho muingia barabarani”
“Ahaaa,wanao pataa ajali ni wale wazembe, utakuta mtu anaendesha pikipiki huku akiwa amekunywa konyagi, sasa ni kwanini asipate ajali”

Anna akalitazama eneo la kituo cha gesi ambacho jana walifanya tukio, na kuwaona baadhi ya askari wakifanya fanya uchunguzi wa vitu vidogo vidogo
“Ahaaa jana hapa kulichimbika” Dereva pikipiki alizungumza
“Kulikuwa na nini?” Anna aliuliza kama vile hajui kilicho tokea
“Ahaa nasikia kuna majambazi walifunga mtaa jana, hapakuwa na askari aliyekurupuka”

“Ahaaaa......!!”
“Ina maana jana hukusikia?”
“Mimi ninatokea,turiani Morogoro na wala sijasikia”
“Ahaaa,jana basi askari wengi wamekufa pale kwa kulipukiwa na gesi”
“Kisa nini hadi wakafa?”
“Ahaaa nasikia kuna sister mmoja ambaye ni jambazi, askari walimshika.Kumbe yule dada ni mafia katika kupambana pambana nao basi akawatoka polisi na sijui alifanyaj fanyaje hadi akailipua mitungi ya gesi”
“Ahaaa masikini weee”
“Ahaaa wee acha tuu, hapo ndipo nimeamini kuwa Tz kuna watu m agaidi kama huko Lebanon”
“Ahaaa pole yao”

Anna akaendelea kuzungumza na muendesha pikipiki hadi wanafika Kariakoo, Anna akatoa noti tatu za elfu kumi na kumkabidhi muendesha pilipiki
“Kaa na chenchi kwani safari ni ndefu”
“Asante dada yangu,Mungu akubariki”
“Amen”
Anna akaingia kwenye duka analo hitaji kununu vifaa na kumuacha muendesha pikipiki akiondoka zake.

Dokta William baada ya kumaliza kikao na viongozi wa polisi, akawaomba wampe muda kuweza kufikiria juu ya ombi lao la kuunda kikosi kipya cha uchunguzi ambacho kitawatafuta majambazi walio sababisha tukio la askari na wananchi kufariki.Kwa bahati nzuri likizo ya Dokta William inaanza sikuinayo fwata, kwa kigezo hichi akatumia kaondoka nchini na kuelekea Israel sehemu ilipo familia yake.

                                             ***

Anna akafanikiwa kununu manunuzi yote aliyo agizwa na wezake, akaelekea sehemu ya kununulia magari ambapo akaanza kutazama ni gari gani ambalo anaweza kununua,kwa bahati nzuri akabahatika kupata gari aina ya corora ambayo imetuka kidogo kwa kiasi cha pesa alicho nacho.

Akamaliza makabidhiano na wauzaji kisha akaondoka na kutafuta baa iliyopo karibu na sehemu ya kuuzia magari, hii ni kuepukana na kukamatwa na askari wa barabarni kwani gari lake bado halijamaliziwa kukamilisha baadhi ya usajili
Akaagiza soda na kunywa kunywa akivuta muda ifike saa mbili usiku aanze safari kurudi sehemu anapoishi, Simu ya ana ikaita na kuona ni namba ya Halima

“Wewe, mbona hurudi?”
“Nipo sehemu nimekaa nasubiri muda uende ende kidogo,kwani barabarani kumechafuka sana”
“Sasa ungesema sio kukaa kimya kutuweka sisi matumbo juu bwana”

“Musijali”
“Hili gari umesha lipata?”
“Ndio”
“Ni zuri au ni kimeo?”
“Zuri kiasi chake”
“Wewe sema zuri kiasi chake, utujie na kimeo hapa utakiendesha wewe mwenyewe”
“Haaa wasi wasi wenu wa nini sasa”
“Powa, jipya?”
“Jipya hakuna ni ishu ya jana ndio top story hapa mjini”
“Ahaaa powa mwaya”
“Ok”

Anna akakata simu na kuendelea kupata kinywaji,hadi in atimu mida ya saa tatu kasoro usiku akalipa pesa ya vinywaji alivyo kunywa na kuingia ndani ya gari,akapitia kwenye moja ya sheli na kujaza mafuta yatakayo mtosha kwa safari.Mwendo wa masaa mawili ukamtosha kufika kwenye handaki lao

“Nice job baby”(Kazi nzuri mtoto)
Rahab alizungumza huku akimpiga piga Anna mgongoni, usiku mzima wakawa na kazi ya kupanga mipango jinsi ya kwenda kuvamia benki ya taifa na muda maalumu walio upanga ni saa sita mchana siku inayo fwata

Kila mmoja akaamka asubuhi akiwa na shauku ya kufanya tukio la kwenda kupora pesa,Fetty akajitolea kuuvaa mwili wa jimama ambalo likambadilisha na kumfanya aonekane ni  mama mtu mzima mwenye familia kubwa.Kila mmoja akajiandaa na kuchukua silaha zake ambazo zitamsaida katika tukio zima,Kabla hawajatoka simu yao ya mezani ikaita 

“Pokea”
Anna akamuomba Rahab kuipokea simu hiyo
“Haloo”
“Dokta Will hapa nazungumza”
“Dokta vipi, mbona umetupiga na simu ya mezani?”
“Hilo halina tatizo sana, kikubwa nataka kuwaambi kuweni makini kwani kuna wanajeshi wametumwa kuja kuukagua huo msitu munapo ishi”
“Lini?”
“Unauliza lini? Wanakuja sasa hivi na wapo njia na hii taarifa nimepewa na kiongozi wao”

 ITAENDELEA....

No comments:

Post a Comment

Sponsor