Advertisement

Breaking

Thursday, September 29, 2016

Serikali Yaridhia Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Bomba La Mafuta


SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. 
 
Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika  tarehe 29 Septemba, 2016  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 
 
Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020. 
 
Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania. 
 
Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda. 
 
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2. 
 
Amebainisha kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya  kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga. 
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi. 
 
Aidha, amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, SEPTEMBA  28, 2016 

No comments:

Post a Comment

Sponsor