Advertisement

Breaking

Wednesday, September 7, 2016

Shaa kufanya show ya kumbukumbu ya kifo cha mama yake Mtwara siku ya Eid, Sept 12

Katika kuadhimisha kifo cha mama yake mzazi aliyefariki August 1 miaka kadhaa iliyopita, Shaa atafanya show mkoani Mtwara, katika sikukuu ya Eid El Haji, Jumatatu Septemba 12.

Alisema kuwa show hiyo pia itakuwa maalum kwa mashabiki wake wa mikoa ya Kusini ambako mama yake anatokea. Pia amesema kuwa kwenye show hiyo itakayofanyika Makonde Beach Club, atatumbuiza pamoja na live band.

Shaa amedai kuwa show hiyo ilitakuwa ifanyike katika wiki ya kuadhiminisha kifo cha mama yake lakini aliombwa aisogeze hadi siku ya Sikukuu.

“Bado ni siku siku nzuri naona ilmradi nitaweza kuonana ana kwa ana na mashabiki wangu huko,” amesema Shaa.
Show hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na kituo cha Radio cha Pride FM ya Mtwara pamoja na Kings Entertainment.

No comments:

Post a Comment

Sponsor