Advertisement

Breaking

Sunday, September 11, 2016

Tundu Lissu Adai Lipumba ni Chanzo cha Vurugu CUF

MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu, amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga wanachama wa CUF.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka  na viti 10.Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheia Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari.
 
Kauli hiyo ameisema jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kuwa kinaivuruga CUF.
Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa matamshi hayo kwa wanachama wa CUF ni chanzo cha yeye kuendelea kukivuruga chama hicho hivyo wanachama wampuuze kwani alikikimbia tokea walipoungana katika umoja wao wa Ukawa kabla ya mwezi mmoja kujiunga  aliyekuwa mgombe urais kupitia umoja huo, Edward Lowasa kupitia Chadema.
Kwa upande mwingine Lissu amesema viongozi wa Chadema wamepanga Jumanne wiki ijayo kupelekea malalamiko yao katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili wafuasi 10 wa Chadema waliokamatwa kwa madai ya kusambaza maneno ya uchochezi.Alisema wanapeleka hoja hiyo mahakamani ili mahakama iweze kuamuru waachiwe huru kwani hivi sasa wanateseka mahabusu.
Alisema mahakama ndiyo chombo kikuu chenye dhamana ya kuwahoji Mkuu Jeshi la Polisi, IGP Ernest  Mangu na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DCI, Diwan Athumani ili watoe sababu ya jeshi la polisi kuwaweka mahabusu wanachama 10 wa chadema kwa zaidi ya wiki moja sasa bila kuwapeleka mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Sponsor