Advertisement

Breaking

Thursday, October 20, 2016

Bavicha waipa serikali siku saba


Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limeipa siku saba serikali kutoa kauli kuhusu ucheleweshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kuitaka serikali ikiri kuwa huo ni udhaifu.
 
Mwenyekiti wa Bavicha Patrobas Katambi amemtaka Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalicako kutolea ufafanuzi suala hilo na kama anaogopa, amuachie Waziri Mkuu au Rais.
 
Amesema endapo watashindwa kutoa kauli hiyo na kuruhusu wanafunzi kurudi nyumbani kwa kushindwa kulipa ada, Bavicha itaungana nao kudai haki yao ya msingi ya kukopeshwa na serikali.

No comments:

Post a Comment

Sponsor