Advertisement

Breaking

Monday, October 17, 2016

Maamuzi ya Umoja wa Ulaya Baada ya Burundi kujitoa Mahakama ya ICC


Siku chache baada ya Burundi kutangaza maamuzi ya kujitoa kwenye Mahakama ya makosa ya uhalifu ICC, Umoja wa Ulaya umetangaza kuitenga serikali ya Burundi kwenye masuala ya fedha za kikosi chake kilichotumwa nchini Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika kusimamia amani nchini humo (AMISOM).

Umoja wa Ulaya, ambaye ni mfadhili mkuu wa Burundi unachangia 20% ya bajeti ya taifa hilo, umeamua kuchukua vikwazo dhidi ya serikali ya Burundi, inayotuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kukataa mpaka sasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani wake. 

Serikali ya Burundi imeendelea kutengwa katika ngazi za kimataifa, na kutuhumiwa uhalifu mbaya dhidi ya binadamu, Umoja wa Ulaya unataka kuzuia moja ya sehemu kuu zinazoipatia serikali ya Burundi fedha za kigeni.

Umoja wa Ulaya umechukua uamuzi wa kutopitisha tena mishahara ya askari wa nchi hiyo wanaosimamia amani nchini Somalia kwenye akaunti ya serikali. 

Uamuzi wa EU unakuja wakati ambao uchumi wa Burundi umeendelea kudorora, hata baadhi ya shughuli zinazoingiza mapato kwa serikali zimekwama kutokana na hali mbaya ya kiuchumi

Ni wiki tatu sasa tangu Umoja wa Ulaya kutuma fedha kwenye akaunti ya Umoja wa Afrika ili kulipa mishahara askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Ripoti kutoka Brussels Ubelgiji zinasema Umoja wa Ulaya umelipa tu malimbikizo ya kipindi kinachoishia hadi Machi 16, 2016, tarehe ambayo Umoja wa Ulaya uliiwekea vikwazo serikali ya Burundi, kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou.

Tangu wakati huo, Umoja wa Ulaya ulisimamisha misaada yake ya moja kwa moja kwa serikal ya Burundi. Ni Euro milioni 5 tu za mishahara ya askari 5,500 wa Burundi wa kikosi cha AMISOM zimekua zikipitishwa kwenye hazina ya serikali ya Burundi.

No comments:

Post a Comment

Sponsor