Advertisement

Breaking

Tuesday, October 18, 2016

Mahakama Yaitupilia Mbali Kesi Ya Mbowe Hotels Dhidi Ya Shirika La Nyumba La Taifa (NHC )

Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa bilcanas.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.

Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.

Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment

Sponsor