Advertisement

Breaking

Sunday, October 2, 2016

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 02 Oktoba, 2016 amemteua Bw. Laston Thomas Msongole kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Bw. Laston Thomas Msongole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Edmund B. Mndolwa ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi wa Bw. Laston Thomas Msongole umeanza  tarehe 02 Oktoba, 2016.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

02 Oktoba, 2016

No comments:

Post a Comment

Sponsor