Advertisement

Breaking

Sunday, October 16, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 25 & 26

MUANDISHI : EDDAZARIA 

ILIPOISHIA....
“Raisi……!!”
Rahab alizungumza baada kwa mshangao baada ya kutokumuona Raisi Praygod kwenye usawa wa bahari jambo lililoanza kumpa wasiwasi mwngi.Ikamlazimu kurudi tena ndani ya maji, kutazama kama anaweza kumuona raisi, ila hakumuuona
“Mungu wangu!!”
Rahabu alizungumza kwa kuhamaki baada ya kuona kitu kikija kwa kasi katika upande aliopo yeye, kwa haraka haraka akagundua kwamba ni samaki mmoja hatari aina ya Papa, ndiye anaye karibia kufika katika eneo alilopo.

ENDELEA.....
Rahab akaanza kujipapasa mwiki mwake kwa haraka, kwabahati nzuri akakikuta kisu kwenye mguu wake wa kulika katika sehemu ya kiatu alipo kichomeka kipindi alipokuwa akivaa, nguo alizo nazo kwenye chumba maalmumu cha kuhifadhia nguo katika ndege ya raisi iliyo anguka muda mchache uliopita.

Akajiweka tayari kwa kupapambana na samaki huyu anaye mfwata kwa kasi katika eneo ambalo  ameangukia, kufumba na kufumbua samaki huyu tayari akawa aweshafika katika eneo alipo Rahab, kwa ustadi wa hali ya juu Rahab akajigeuza ndani ya maji na kushuka kwa kasi ndani ya maji, na kusababisha samaki huyu mkubwa kupita juu yake, kwa kasi jambo lililo zidisha ukali wa samaki huyu mwenye uchu wa kutafuna kiumbe chochote kitakacho ingia kwenye enoa la bahari alipo yeye

Rahab akakishika vizuri kishu chake chenye ncha kali, na kutazama jinsi samaki huyu anavyo kunja kona na kurudi katika eneo alipo kwa kasi kubwa, samaki akamfikia Rahab kwa karibu kabla samaki hajafanya maamuzi ya aina yoyote, Rahab akamuwahi kumchoma kisu kwenye eneo la tumbo la samaki huyu, lenye ngozi laini na kuanza kulichana kwa kutumia nguvu nyingi, jambo lililo sababisa damu nyingi kutapakaa katika enoa la sehemu walipo, huku utumbo mwingi wasamaki huyu ukitapakaa kwenye maji
“Haaaaaaaa”

Rahab alizungumza huku akichomoza kichwa chake kwenye maji, huku akivuta pumzi kwa wingi, akajilegeza mwili wake na kuufanya uanze kuelea elea juu ya maji, huku akitazma juu mwili wake ukiwa umechoka sana
                                                                                                  Agnes akamgeuza mtu aliye anguka na kumchunguza vizuri na kugundua kwamba anamajeraha kadhaa kwenye mwili wake, Agnes akapiga mluzi ulio mfikia Halima aliyekuwa katika eneo la karibu, Halima akapa hatua za haraka hadi katika sehemu alipo simama Agnes
“Best kuna mtu hapa nimemuona”

Agnes alizungumza huku akimgeuza mtu aliye lala chini huku damu zikimvuja, Halima akamtazama mtu aliye lala chini kwa umakini, pasipo kuzungumza kita cha aina yoyote, kiasha akaikoki bastola yake akiziweka risasi zilizopo kwenye magazine yake, kuwa tayari kutoka nje, kitu kikubwa alicho kibakisha ni kuivuta traiga ya bastola yeka kuziruhusu risasi atakazo zihitaji kutoka nje

“Halima unataka kufanya nini?”
“Hastahili kuishi, mtu mwenye ni mfu huyu”
“Hembu ngoja kwanza?”
“Nini?”
“Usimuue?”
“Sasa anabaki duniani wa kazi gani, unamtambua huyu mtu”
Halima alizumgumza kwasauti iliyo jaa msisitizo mwingi
“Hata kama, simfahamu ila kuna kitu ninacho kihisi kwa huyu jamaa”

“Kwanza ametokea wapi?”
“Mimi sifahamu, ila nilisikia kishindo, nilipo kuja hapa ndipo nilipo muona huyu jaamaa akiwa amelala hapa”
Halima pasipo kuuuliza akafyatua baadhi ya risasi, jambo lililo muudhi sana Agnes na kumfanya amsukume Halima na kuangukia pembeni

“Mbona unakuwa mpumbavu wewe, nini unafanya”
Agnes alizungumza kwa hasira huku akimfokea kwa nguvu Halima aliye angukia pembeni, kwa bahati nzuri risasi alizo zifyatua Halima alizipiga pembeni ulipo mwili wa jamaa na hapakuwa na risasi iliyo ingia katika mwili wa mtu waliye muona.

Milio ya risasi ikawastua Fetty pamoja Anna ikawalazimu kutoka nje ya ‘submarine’ na kuelekea sehemu walipo isikia milio ya risasi huku wakiwa makini sana, kila mmoja akiwa ameishika bastola yake mkononi, waakawakuta Agnes na Halima wakiwa wanafokeana huku kila mmoja akionekana kuwa na jazba ya ajabu, Fetty akafyatua risasi mbili hewani nakuwafanya  Agnes na Halima kunyamaza
“Nyingi mumechanganyikiwa?”
Fetty aliuliza kwa sauti juu huku akiwatazama Halima na Agnes

“Si  ninazungumza na nyinyi, hamuoni shida tulizo nazo ila bado munagombana kwa kitu kipi?”
Halima hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuondoka na kuwaacha wezake wakimtazama kwa macho yaliyo jaa mshangao mwingi
“Agnes kuna nini?”
Anna aliuliza  huku akimtazama Agnes aliye fura hasira nyingi 

“Kisa ni hyo jamaa aliye lala chini hapo”
Fetty akapiga goti moja chini na kumshika shingo, mtu aliye anguka chini ya akiwa anavujwa na damu za puani
“Ametokea wapi?” Fetty aliuliza
“Sifahamu, ila nimemuona akiwa ameanguka tu”
“Ameanguka kutoka wapi?”
“Kutoka juu”
“Juuu?”
“Ndio”
“Hembu shika huko”

Fetty alimuomba Anna kuweza kumshika mtu aliye anguka katika eneo la miguu, kwa kusaidiana wote watatu wakamnyanyua juu, na kumpeleka ilipo manohari, wakamuingiza ndani na kunaza kumfanyia huduma ya kwanza, jambo lililo zidi kumkera Halima ambaye hakuhitaji kumuona mtu asiye mfahamu akiwa upende wao
“Raisi”

Rahab alizungumza huku akiingiza miguu yake kwenye maji, na kubakisha kiwiliwili cha juu na kuanza kuangaza kila kona ya eneo alilopo ila hakumuona Raisi Praygod, umbali kidogo kutoka katika sehemu alipo, akaona miti mingi ikiashiria kwamba kuna kisiwa, akavuta pumzi nyingi na kunza kuogelea huku akiendelea kutazama kila eneo, akihisi kwamba anaweza kumuona muheshimiwa raisi, hadi anafika kwenye ukingo wa bahari, ambapo emetumia takribani dakika ishirini na sita kufika alipo, akiajilaza kwenye mchanga mwingi, wenye rangi nyeupe huku akiwa wamechoka mwili wake kupita maelezo
“Ohooo mama yangu nakufa mie”

Rahaba alizungumza huku akihema mithili ya bata mzinga aliye kimbia kwa umbali mrefu, akajilaza kwa dakika kumi, kisha akasimama na kutazama kila upande wa kisiwa hichi, chenye miti mingi mirefu iliyo fungamana kwa ukaribu, na kwambali kukiwa na sauti nyingi za ndege wenye milio mizuri
“Hapa ni wapi?”

Alizungumza huku akitembea tembea katika eneo hili lenye mchanga mwingi wa bahari, ambao kwa mtu aliye choka humuwia ugumu mwingi kutembea, njaa kali haikucheza mbali katika tumbo la Rahab, kila jinsi anavyozidi kwenda mbele ndivyo jinsi alivyoaanza kujihisi mwili kunyong’onyea na kumuishia nguvu, kwa mbali akaliona koti jeusi ambalo alikuwa amelivaa Raisi Praygod Makuya likiwa pembezoni mwa bahari, akapiga hatua za kiuvivu uvivu hadi lilipo koti na kuliokota, akatazama kila upande na hakuuona mwili wa Raisi, akiwa amesimama akasikia sauti ya mtu akikohoa kwenye moja ya kifusi kikubwa kilicho hatua chache kutoka sehemu alip simama, akakimbia hadi kilipo kifusi na kumkuta Raisi Praygod Makuya akiwa amefunikwa na mchanga mwingi wa kuanzia tumboni hadi miguuni huku maji yakiendelea kuipiga miguu yake taratibu na kurudi baharini
 
Kitendo cha kuzama ndani ya maji, baada ya kudondoka kutoka kwenye maji, raisi Praygod Makuya akanyanyuliwa na wimbi kubwa lililoanza kumpeleka usawa wa kisiwa, kwa uzito wa maji na kasi yake kubwa, akajikuta akiupwa pembezoni na bahari, mchanhg mwingi ukamfunika, huku koti lake likipelekwa na maji na kukwama kwenye moja ya vimawe mawe vilivyoopo pembezoni mwa bahari, baada ya jua kali lililokuwa likimpiga usoni mwake, ufahamu ukaanza kumrudia na kujikuta akianza kukohoa taratibu taratibu, gafla akahisi mtu akimgusa, akayafumbu macho yake yaliyo jaa ukungu mwingi, kwa mbali aliweza kuiona sura ya Rahab, ila kutokana na ukungu ilio tanda kwenye macho yake hakuwa na uhakika kamili kama ni Rahab mwenye au ni mtu mwengine

“Raisi”
Sauti ya Rahab ikumuita ikaanza kumpa matumanini na kuamini kwamba ndio Rahab mwenyewe aliye muita.
“Ni mimi Rahab”

Rahab alizungumza huku akiendelea kuutoa mchanga ulio mfunikaka Raisi, akafanikiwa kumaliza kuutoa mchanga wote, akaishika mikono ya Raisi na kumnyanyua juu, raisi akafanikiwa kumuona Rahab vizuri na kujikuta akiachia tabasamu pana usoni mwake
“Asanye binti”
“Sa…”

Kabla Rahab hajamaliza sentensi wake wakastukia kuona kundi kubwa la watu walio valia ngozi za wanyama wa msituni, wakija kwa kasi katika sehemu walipo simama huku wakipiga vigelele gele na mikononi mwao wakiwa wameshika minyale na mikuki mingi, wakiashiria kwamba wapo tayari kwa kuwashambulia Raisi na Rahab, ambaye amejipapasa mwili mzima na kujikuta akiwa hana silaha hata moja
*****Je watasalimika mikononi mwa hawa watu, usikose toleo lijalo hapa hapa kwenye hii page****
            
             SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……26

Watu hao wakawazingira Rahab na Raisi Praygod, huku wakiendelea kupiga kelele za ajabu, pamoja
huku mikuki na mishale yao wakiielekezea kwa Rahab na Raisi Praygod
“Binti kuwa mpole”

Raisi Praygod alizungumza huku akiinyoosha mikono yake juu, Rahab naye akatii kunyoosha mikono yake juu, jamaa wawili wenye misuli wakawasukuma Rahab na Raisi Praygod, wakaanguka chini, wakafungwa kamba za miguuni na mikononi, kisha wakanyanyuliwa na kubebwa juujuu, wakipelekwa wasipo pafahamu. 

Wakafikishwa kwenye moja ya kijiji chenye watu wengi, huku nyumba zao zikiwa zimetengenezwa kwa nyasi pamoja na miti, hazikuwa na urefu sana, kwenda juu, huku milango yao ikiwa ni midogo katika sehemu ya kuingilia.Rahab na Raisi Praygod, wakafungwa kwenye moja ya mti mkubwa, huku miili yao ikizungushiwa kamba ngumu, iliyo zunguka kwenye mti huo.

 Giza likaingia pasipo, kujua ni kitu gani kinacho endelea, watu hawa wenye kuzungumza lugha ya ajabu, hawakuwa na muda kabisha na Rahab pamoja na Raisi Praygod, kila mmoja anaonekana kuwa bize na shughuli yake, wakaanza kusikia mlio wa ngoma, ulio changanyikana na kelele za ajabu, ikionekana watu hao wakiwa wapo katika kusherehekea

“Hawa ni watu gani?”
Ragab alimuuliza Raisi Praygod
“Hata mimi sifahamu, ndio mara yangu ya kwanza
kuwaona watu wa aina kama hii”

Wakastukia kuona kundi kubwa la wanaume wakija huku mikononi mwao wakiwa wameshika miti ambayo juu yake imefungwa matambaa yanayo waka kwa moyo mkali.Wakawafungua na kuwabeba juu juu kama walivyo waleta pale awali, wakatupwa chini pembezoni mwa jungu kubwa lililo wekwa kwenye mafiga matatu, huku likitoa mvuke mwingi, ikiashiria kuna maji mengi yanayo chemshwa.

 Macho ya Rahab yakawa na kazi ya kutazama watu walio wazunguka, wanawake wa watoto, wakiendelea kushangilia, huku waume zao wengine wakipiga ngoma, huku wengine wakiwa na kazi ya kuhimarisha ulinzi uliopo kwenye eneo hili, akasimama mzee mmoja aliyekuwa amekalia kiti kilicho tengenezwa kwa ngozi ya chui.Mwili wa mzee huyo anaye onekena ni mkubwa sana kiumri, umevishwa dhahabu nyingi kuanzia kichwani hadi miguuni, zilizo tengenezwa katika mionekano tofauti ya hereni, cheni na bangili. 

Ukimya ukatawala baada ya mzee huyo kunyanyua mikono yake juu akishiria watu wote kukaa kimya.Akawatazama Rahab na Raisi Pyaygod ambao, wamelala chini huku nguo zao zikiwa zimechafuka kwa vumbi jingi lililopo katika sehemu hiyo.

“Lajmet e juaj?”(Habari zenu)
Mzee huyo aliwasalimia watu wake kwa saut ya upole nyenye kukwaruza kwaruza
“Wanazungumza lugha gani?” Rahab aliuliza
“Wanazungumza ki Albania”
Raisi alijibu kwa sauti ya chini huku akimtazama mzee huyo
“Te sigurt Pergjithshem”(Salama mkuu)
Watu wote walijibu kwa pamoja huku wakiinamisha vichwa vyao chini, kama ishara ya kumuheshimu
mzee huyo

“Sot eshte nje dite e mire dhe e kendshme”(Leo nisiku nzuri ya kupendeza)
“Ku gjalle yne I ri na kane sjelle ushgimin me te mire per shendetin tone”(Ambapo vijana wetu, mahiri wametuletea chakula bora kwa afya zetu)
Raisi Praygod akastuka baada ya kusikia chakula bora, kwa mahesabu ya haraka haraka yaliyo mjia
kichwani anatambua kwamba chakula kinacho zungumziwa hapo si kingine ila ni miili yao

“Hawa watu wanakula nyama za watu”
“Nini?”
“Ndio, hapa wapo kwenye mikakati ya kutaka
kutula sisi nyama”
“Mungu wangu”
Japo kuna hali ya ubaridi ila kajasho kembamba kakaanza kumchuruzika raisi Praygod, huku
mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio, akili ya Rahab ikaanza kufanya kazi kwa haraka akijaribu kutafuta jinsi ya kujiokoa kutoka mikononi mwa watu hao.Akatazama kila sehemu, hakuona

sehemu yoyote yenye upenyo wa kutokea, wanume wanne walio jazia miili yao kwa misuli iliyo
kakamaa, wakasimama pembeni ya Raisi Praygod na Rahab, huku wakiwa wamevali ngozi za
wanyama na mikononi mwao wakiwa na visu vikali wakisubiria kupata amri kutoka kwa mkuu wao
“Eshte koha tani per te vlim ushgimin tone”(Ni wakati sasa wa kuchemsha chakula chetu)

Mzee huyo alitoa amri kwa vijana wake, na kuwafanya watu waliopo katika eneo hilo kushangilia kwa furaha, huku vijana hao wanne wakianza kuzikata kamba walizo wafunga Rahab na Raisi Praygod tayari kwa kutatumbukiza katika jungu hili kubwa, lenye maji yanayo chemka sana
 
Kwa dawa walizo mpatia mtu waliye muokota, zikaanza kuzaa matumaini kadri masaa yalivyo zidi kukatika, mtu huyo akaanza kupata nafuu iliyo pelekea kuyafumbua macho yake kutazama ni wapi alipo

“Unaitwa nani?”
Fetty alimuuliza mtu huyo, anaye onekena kuendelea kushangaa shangaa ndani ya chumba alipo, akatazma akila pande, nakuona wasichana watatu wakiwa wamesimama pembeni yao, huku wakiwa na bastola kwenye viuono vyao, akataka kunyanyuka ila Anna akamuwahi kumrudisha kitandani

“Tulia, upo sehemu salama, je unajua kuzungumzaKiswahili?” Anna alimuuliza
“Ndio”
Mtu huyo alijibu kwa sauti ya chini na kuwafanya, Anna kuwatazama wezake
“Unaitwa nani?”
Anna alimuuliza tena mtu huyo
“Sa….m”
Alijibu kwa kifupi, huku akionekana kupata shida sana katika kuzungumza kwake
“Sam, ndio nini?” Agnes aliuliza
“Samson”

“Ahaaaa, umetokea wapi?” Fetty aliuliza
“Munamuuliza maswali mengi ya nini?”
Sauti ya Halima ilisikika kutoka mlangoni, alipo simama akiwatazama wezake hawa wanamshuhulikia mtu waliye muokota, Fettyakamtazama Halima kwa macho makali kisha akaachia msunyo mkali, akishiria kukasirishwa na swali la Halima

“Halima ninakuomba utoke humu ndani?”
Fetty alizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa ukali fulani ndani yake
“Eheeeee,”
Halima alicheka kwa dharau huku akipiga hatua za taratibu na kuondoka katika chumba walipo wezake
“Ana nini, huyu?”
Agnes aliuliza huku akimtazama Halima anaye potelea mbele ya macho yao
“Hembe, tuweni makini naye, Sawa?” Fetty alizungumza
“Sawa”

Halima, akaelekea moja kwa moja katika chumba walichopo manahodha wa nyambizi(submarine) hii,
akawakuta wakiwa wanajaribu kutafuta mawasiliano kisiriri siri, ili kuweza kujitoa mikononi mwa hawa watekaji, walio waua wezao bila yahuruma, Halima akawatazama kwa umakini, pasipo wao kugundua uwepo wa Halima katika chumba hichi, ambaye amesimama nyuma yao

“One, nine, nine, nine Over”(1, 9, 9, 9, Over)
Nahodha mmoja alizungumza kwa kupitia kifaa maalumu cha mawasiliano, huku mwenezake
akionekana kuhangaika na simu kubwa iliyo jaa batani nyingi
“I repeat One, nine, nine, nine. Over”(Ninarudia, 1,9,
9, 9, Over)
Halima akaendelea kuwatazama jinsi manahodha hawa wanacho kifanya, akatoa bastola yake, akatoa magazine na kukuta risasi za kutosha
“Hei….”

Halima alizungumza na kuwastua manahodha hao, pasipo kuwa na huruma, Halima akafyatua risasi
moja iliyotua kichwani mwa nahodha mkuu ambaye alikuwa akihangaika kuminya minya batani nyingi zilizopo kwenye simu hii ya kijeshi, inayo tumika kwa mawasiliano ya masafa marefu
“Endelea……”

Halima alimuambia nahodha msaidizi, ambaye mwili mzima umeanza kumtetemeka kwa woga baada ya kumuona mkuu wake akiwa ameanguka chini, huku damu zikiwa zinamvuja kwenye kichwa chake, na taratibu akiiaga dunia. Mlio wa risasi, ukawastusha Fetty na wezake walipomo kwenye chumba cha kuhudimia wagonjwa, kwa haraja Fetty akatoka pamoja na Anna kwenda kutazama ni nini kilicho tokea huku, Agnes akibaki na mgojwa.Wakamkuta Halima akiwa amemnyooshea nahodha msaidizi bastola, huku nahodha mkuu akiwa ameanguka chini, akiwa amepoteza maisha tayari

“Weka bastola yako chini”
Fetty alizungumza kwa msisitizo huku bastola yake akiwa amemnyooshea Halima, Halima akamgeukia Fetty na kumtazama kwa macho ya mshangao

“Halima, sinta rudia nimekuambia weka bastola yako chini, kabla sijausambaratisha ubongo wako”
“Khaaaa, Fetty unatania eheee…!?” Halima aliuliza kwa mshangao
“Halima sitanii, moja, mbili,………..”
Halima akaitupa chini bastola yake, na kuipiga teke, akimsogezea Fetty sehemu alipo simama, Anna akaiokota bastola ya Halima, kisha akapiga
hatua hadi sehemu alipo anguka nahodha mkuu “Ameshakufa”

Anna alizungumza baada ya kuuweka kiganja chake kimoja kwenye kifua cha nahodha huyo
“Kwanini umemuua?”
Fetty aliuliza kwa hasira, huku bastola yake akiinyooshea kwa Halima, anaye onekana kuto kustushwa na tukio lililo tokea mbele yao
“Nakuuliza wewe, Malaya kwanini umemuua huyu mzee?” Fetty aligomba

“Mimi Malaya?”
“Ndio wewe, Malaya tena uliye kubuhu”
Halima akacheka kicheko cha dharau na kuanza kupiga hatua za kuelekea mlango wa kutoke nje ya chumba hicho
“Simama, ukipiga hatua ninakuua”

Fetty alizungumza kwa msisitizo, Halima akasimama, taratibu akageuka na kumtazama Fetty, akapiga hatua za taratibu hadi sehemu alipo simama Fetty, kisha kwa hasira akishika bastola ya Fetty na kuilekeza kwenye paji la uso wake, huku akiigandamiza kwa nguvu zake zote
“Si unataka kuniua? Niue sasa”

Halima alizungumza kwa hasira huku ameyang’ata meno yake, akimtazama Fetty anaye tetemeka kwa hasira kali, iliyo pelekea sura yake kukunjana na kutisha mithili ya chui jike, aliye uliwa watoto wake akishuhudia.Gafla mlio wa risasi ukasikika huku kishindo kikubwa cha mtu kuanguka chini kikisikika
ndani ya chumba walichomo....
                                                                             ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Sponsor