Advertisement

Breaking

Thursday, October 20, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 27 & 28


MUANDISHI : EDDAZARIA 

ILIPOISHIA
“Si unataka kuniua? Niue sasa”
Halima alizungumza kwa hasira huku ameyang’ata meno yake, akimtazama Fetty anaye tetemeka kwa hasira kali, iliyo pelekea sura yake kukunjana na kutisha mithili ya chui jike, aliye uliwa watoto wake
akishuhudia.Gafla mlio wa risasi ukasikika huku kishindo kikubwa cha mtu kuanguka chini kikisikika
ndani ya chumba walichomo.

ENDELEA
Wote macho yao wakayapeleka sehemu alipo angukia mtu huyo, aliye pigwa risasi na kukuta ni yule nahodha msaidizi akiwa chini amelala huku, damu zikimtoka kifuani mwake na kwenye mkono wake wakulia akiwa ameshika bastola ikiashiria kwamba alitaka kuwashambulia wote waliomo ndani ya chumba ila Anna alimuwahi.
 
Halima akatoka na kuwaacha wezake kwenye chumba walichopo, akatoka nje ya manohari na kupanda juu kabisa, akawasha sigara yake taratibu na kuanza kuvuta, huku  akijaribu kuishusha hasira yake iliyo tokana na wezake kumuamini Samson, ambaye hataki hata kumuona kwenye macho yake.
                                                                                           *********
Rahab na raisi Praygod Makuya walipo malizwa kufunguliwa kamba zao kwa ajili ya kudumbukizwa kwenye jungu kubwa lenye maji yaliyo chemshwa kwa ajili yao. Rahab akamkonyeza muheshimiwa raisi na hapo hapo, wakaanza kupambana na vijeba hivyo vipatavyo sita, na kuwafanya watu wengine walio kusanyika katika eneo la uwanja kushuhudia kuuawa kwao, ili wawale wakaanza kuchanganyikiwa kwani kwa mapigo aliyo kuwa akiyapiga Rahab, yalimshangaza hadi chifu wao, hakuamini kuona mtoto wa kike akipambana kwa kiasi cha kuwaangusha vijeba wenye miraba miine.
“Twende muheshimiwa”
 
Rahab alizungumza baada ya kupata kijinafasi cha kukimbia kutoka kwenye kundi kubwa la watu hawa. Wakaanza kukimbia kuiingia msituni huku wakifwatwa kwa nyuma na kundi la askari wa kijiji hichi ambao wanatumia mishale na upendi katika kuwashumbulia. Kila walivyo kimbia ndivyo kundi la askari hao lilvyo zidi kuwafukuzia, na mbaya zaidi, mwanga wa mbalamwezi ulimulika kila upende wa anga na kuwafanya washinde kujificha kwenye vichaka kuhofia kuonekana na kukamatwa tena.
“Nimechoka…..”
 
Raisi alizungumza huku akionekana kukatishwa tamaa na kukimbia huko, Rahab akamshika mkono raisi na kuendelea kukimbia, kwa bahati nzuri wakakuta moja ya pango, wakaingia pasipo kuchunguza ndani ya pango hili kutakuwa na kitu gani. Askari hao waliokuwa wanawakimbiza wakapita kwa spidi katika pango hilo pasipo kuchunguza sana kama watu wanao wakimbiza watakuwa wameingia ndani ya pango hilo.
“Asante tena binti”
 
Rahisi alizungumza huku akiendelea kuhema kwa fujo, akionekana dhahiri kwamba hakuwa ni mtu wa mazoezi. Hawakuwa na sababu ya kuendelea kukaa tena ndani ya pango hilo baada ya kikundi hicho cha askari kupita kwa kasi katika eneo hilo. Wakabadilisha muelekeo na kupita katika njia tofauti na walio kwenda askari hao, ambao laiti wakitiwa mikononi basi hukumu yao ni ile ile ya kwenda kutafunwa nyama. Usiku mzima wakautumia kukimbia, na kutembea pale ilipo walazimu kufanya hivyo, hadi kunapambazuka bado wapo kwenye msitu huu ambao hawaelewi wanaweza kujitoa.
“Tunaweza kupumzika sasa”
 
Rahab alimuambia muheshimiwa Raisi, baada ya kupata eneo lililo tulia na lina maficho ya wao kupumzika. Raisi Praygod hakuwa na kipingamizi zaidi ya kutafuta sehemu na akajibwaga kama mzigo, miguu yake yote ikawa inawaka moto kwa jinsi alivyo kimbia na kutembea kwa muda mrefu, akavivua viatu vyake na kuviweka pembeni kisha akajilaza.
 
Rahab akasimama na kuanza kulichunguza eneo zima, kuhakikisha kama wanaweza hata kujilaza kidogo katika sehemu hiyo pasipo buguzi. Akiwa katika kuchunguza chunguza sehemu akabahatika kupata kuona mti wenye matunda mengi makubwa na mazuri, akausogelea na kulichuma tunda moja, akalipasua na kulilamba. Akapata laza tamu ya tunda hilo ambalo hakujua ni tunda la aina gani. Akaanza kulitafuna taratibu kusikilizia kama kuna madhara yoyote atakayo yapata, ila haikuwa hivyo kadri jinsi alivyo zidi kulila ndivyo jinsi alivyo zidi kunogewa na tunda hilo, na wala hakusikia mabadiliko yoyote katika mwili wake. Akachuma mengi kidogo na kurudi sehemu alipo lala muheshimiwa raisi Praygog.
 
“Muheshimiwa amka”
Rais akajinyanyua kivivu na kukaa kitako, huku akipiga miyayo, akiashiria kwamba yupo katika hali ya uchovu mkubwa. Rahab akampa tunda moja muheshimiwa kwa ajili ya kupunguza njaa ambayo inaendelea kukwangua matumbo yao, muheshimiwa raisi akaanza kula matunda hayo.
“Matunda gani haya?”
 
“Mimi wala sijui ni matunda gani nimeyachuma hapo mbele”
“Aiseee nimatamu sana, sijawahi kula matunda matamu kama haya”
“Yapo mengi, nikayachume mengine?”
“Twende tukachume”
 
Raisi akavaa viatu vyake na kwenda ulipo mti huo wenye matunda, wanayo kula. Wakaanza kuyachuma na kuendelea kuyala. Wakiwa katikati ya kuyashambulia matunda hayo, kwa mbali wakaisikia milio ya mingurumu ya magari.
“Ina maana hapa kuna barabara?”
Raisi alimuuliza Rahab, ambaye aliacha kutafuna tunda alilo kua kitafuna kipande kidogo ndani ya mdomo wake na kusikilizia sauti ya mingurumo hiyo ya magari ni wapi inapo toke.
 
“Ndio nahisi kuna sehemu ipo barabara”
“Twende tuiwate”
Wakabeba matunda ya ziada, na kuanza safari ya kufwatisha inapo tokea milio hiyo ya magari, haikuwa safari ndogo kuitafuta barabara hiyo inayo pitisha magari, ili waweze kuomba msaada wa kuweza kuwafikisha wanapo kwenda. Ikawachukua zaidi ya lisaa zima, kufika wanapo sikia milio hiyo ya magari. Haikuwa ni barabara kama walivyo zania, wakakuta uwanja mkubwa ambao una watu wengi walio jichora michoro tofauti tofauti kwenye miili yao, huku wakiwa uchi, wanaume kwa wanawake. Magari yao hayakuwa ni magari kama waliyo yazea kuyaona yanayo tumiwa na watu wa kawaida. Magari yao yametengenezwa kwa vyuma vigumu na yana miundo ya ajabu, na mengi yanafanania na magari yaliyo tumika katika filamu ya ‘DEATH RACE’.
 
Michezo iliyo kuwa inafanywa na watu hao wasio na aibu hata kidogo, baadhi yao kushindana na magari yao kwenye uwanja wao kwa mtindo wa kugongana magari
“Hawa ni watu gani…….!!!?”
 
Rahab aliuliza huku akiwa ameshangaa, kabla raisi hajajibu kitu chochote wakastukia risasi ikipiga kwenye mti walio kuwa wamejibanza wakishangaa kundi hilo la watu, wasijue ni wapi risasi hiyo imetokea
                                                                                                 ********
Hali ngummu ya hali ya hewa ya baridi kali, ikaendelea kuuimiza miili ya Fetty, Halima, Anna, Agnes na Samson, walio jifungia ndani ya manohari kwa siku kadhaa wakisubiria barafu lililo ganda baharini kuyayuka na kuendelea  na safari yao, huku Samson akiwaeleza yeye ni mtaalamu mkubwa wa kuendesha vyombo kama hivyo.
“Sijui Rahab kwa sasa yupo wapi best yetu”
 
Agnes alizungumza, wakiwa wamekusanyika pamoja kwenye chumba, chenye joto kidogo kwani hali ya nje ya chombo chao ilizidi kuwa mbaya sana. Samson akastuka baada ya kulisikia jina la Rahab, ila akajikausha kukaa kimya ili asistukiwe, kwani yeye anajua yote yaliyo tokea kati yake na Rahab.
 
“Sijui amekufa au yupo mafichoni?”
“Weee Rahab si rahisi kufa kwa maana namkubali”
“Ila itabidi tufanya mpango wa kujikomboa huku, ili tuweze kumpata mshikaji wetu kwa maana anasiri zetu nnyingi na endapo hatuta mpata siku akitiwa mikononi inaweza kuwa hali ngumu kwetu”
 
“Kama sisi tulikamatwa basi, hatukuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote sidhani kam Rahab anaweza kuzungumza chochote pale atakapo kuwa amekamatwa”
Fetty na wezake wakaendelea kuzungumza, ila Samson hakuchangia chochote juu mada inayo muhusu Rahab
                                                                                                 *******
Hali ya masikitiko ikaendelea kuzizimi katika nchi ya Tanzania, hii ni wananchi kuiona taartifa ikionyesha ndege ya raisi kwamba imetekwa na magaidi na kutegwa bomu lililo lipuka, wakilishuhudia kupitia televishion zao. Kitu kilicho zidi kuwachanganya viongozi wa serikali ni pamoja na mabaki ya ndege yaliyo onekana katika bahari na Pasific, yakielea elea juu ya maji, huku kukiwa hakuna mtu hata mmoja aliye weza kusalia kwenye ajali hiyo, iliyo wahuzunisha watu wengi si wananchi wa Tanzania peke yao bali hata mataifa majirani waliweza kuguswa na kifo hicho cha Raisi Praygod Makuya na watu wake.
 
“Ndugu wananchi, kwa masikitiko yaliyo makubwa, ninatangaza siku kumi na nne za maombolezo ya raisi wetu pamoja timu yake, waliop pata ajali kwenye ndege. Iliyo shambuliwa na…….”
 
Sauti ya makamu wa Raisi, ilisikika katika vyombo vyote vya habari, Redio na Tv. Kila mwananchi hakusita kujiweka karibu na kitu ambacho alihisi kinaweza kumpatia habari juu ya tukio zima. 
 
Wenye maduka, maofisi, mashule na kadhalika, waliweza kuzisimamisha kazi zao kufanya maombolezo ya kifo cha raisi wao mpendwa ambaye alikuwa bado ni kijana mdogo sana mweney umri wa miaka thelethini na tano.
 
Mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa kimya, hata mtaa wa Kariakoo, unaosifika kuwa na watu wengi, katika siku zote za wiki, ulitawaliwa na ukimya wa hali ya juu, watu wengi wanakumbuaka hali kama hii ilisha wahi kujitokeza mwaka 1999, alipo fariki Raisi wa kwanza, ambaye ni baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius K.Nyerere.
                                                                                                   **********
Kiwewe cha risasi iliyo piga kwenye mti kikazidi kuwachanganya Raisi Praygod Makuya na Rahab, ambao walitazama kila kona ya sehemu walipo ila wasione mtu anaye walenga kwa silha. Watu walio kwenye uwaja, wakaendelea na mashindano yao kama kawaida, wasijali mlio huo wa bunduki. 

Risasi zikaanza kumiminika katika eneo walilo jificha Rahab na Raisi Praygod Makuya. Ikawalazimu kuanza kukimbia kuelekea ulipo uwanja, kwani risasi hizo zilikuwa zikitokea nyuma yao, kulipokuwa walenga shabaha wapatao wanne wanao linda uwanja huo, cha kushangaza zaidi nao wapo uchi kabisa, lengo lao halikuwa si kuwaua Rahab na raisi Praygod, ila walihitaji kukajumuike na wezao wanao endelea na michezo hiyo.
 
Rahab na raisi Praygod wakajikuta wakiwa wamesimama kwenye uwanja huo, watu wote waliopo kwenye uwanja huo wakakaa kimya wakiwashangaa kwa jinsi walivyo valia nguo zao.
“Muheshimiwa hapa tutafanyaje?”
 
Rahab alizungumza huku akihema sana kwa wasiwasi akiwatazama watu hawa wanao onekana kama wametokea kuzimu, hii ni kutokana na michoro ya ajabu waliyo ichora kwenye miili yao.
“Tuvue nguo”
Raisi alizungumza huku, akianza kufungua vifungo vya shati lake jeupe lililo chafuka hadi, limepoteza taswira nzuri ya muonekano wake kama lilivyo kuwa hapo awali.
                                                                                   
SHE IS MY WIFE(28)

Wote wakajikuta wakiendelea kuchojoa nguo zao hadi wakabaki watupu, chakushangaza hapakuwa na mtu aliye onekana kuwajali kwa kitendo walicho kifanya zaidi ya watu hao kuendelea kushangilia mashindano yao ya magari. Raisi Praygod akamshika mkono Rahab na wakakatiza katikati ya kundi la watu hao, hadi wakatokea upande wa pili wa uwanja na kundelea kukimbia kwenda wasipo pafahamu,
“Nguo!?”
 
Rahaba alizungumza kwa mshangao mkubwa huku akihema sana. Raisi hakuwa hata na muda wa kuzifikiria nguo zake. Alicho kifanya yeye ni kuendelea kupumua kwa nguvu huku mikono yake akiwa ameshika magotini mwake. Wakaendelea kujipumzisha kwamuda hadi walipo pata nguvu nyingine ya kuendelea kupiga hatua kusonga mbele.
 
Hakuna ambaye aliweza kumtamani mwenzake zaidi kila mmoja alicho kifikiria kwa muda huo ni jinsi gani wanaweza kutoka ndani ya msitu huo wenye hali ngumu ya kutisha. Kwa bahati nzuri wakafanikiwa kufika kwenye moja ya kijiji, majira ya saa tatu usiku, kutokana na mwanga wa mbalamwezi waliweza kuzihesabu vijumba vichache vipatavyo kumi na mbili, vilivyo tengenezwa kwa mbao. Kwa mwendo wa tahadhari wakakatiza kwenye nyumba hizo ambazo zinaonekana hazina uwepo wa watu ndani.
 
Wakasikia sauti ya luninga ikitokea kwenye moja ya nyumba kati ya hivi vinyumba vilizopo, kwa mwendo wa tahadhari wakakisogelea kijumba chenye kusikika sauti ya kubinga hiyo, wanayo hisi kuna mechi ya mpira wanatazama. Wakachungulia dirishani huku wakionekana kuwa na wasiwasi mwingi kwani hapakuwa na aliye kuwa na uhakika kama kuna usalama katika sehemu waliyopo.
“Mbona ndani hakuna mtu”
 
Rahab alizungumza huku akichungulia ndani kupitia kajidirisha ka kioo, kilicho jaa vumbi jingi.
“Hembu tazama tazama vizuri”
“Kweli muheshimiwa ndani hakuna mtu”
“Hembu tuzunguke kwenye mlango”
Wakazunguka hadi kwenye mlango, Rahab akataka kugonga ila Raisi Praygod akawahi kumzuia asifanye hivyo, taratibu Raisi Praygod akausukuma mlango na wakaingia ndani huku wote wakionekana kuwa makini kwa lolote litakalo jitokeza mbele yao.
 
Wakafanikiwa kuingia ndani, cha kushangaza hawakuweza kumkuta mtu yoyote zaidi ya luninga hiyo inayo toa sauti kubwa, huku ikiwa imejawa na vumbi jingi sana.
“Nahisi watu walio kuwa wanaishi hapa walishahama siku nyingi”
Raisi Praygod alizungumza
“Unauhakika gani kumeshimiwa kama watu hao watakuwa wamehama siku ningi?”
“Tazama mazingira ya humu ndani jinsi yalivyo jaa vumbi jingi, nilazima watakuwa wamehama siku nyingi”
Wakaendela kutazama kila chumba ila hawakufanikiwa kuweza kuona mtu yoyote zaidi ya vitu vilivyomo humu ndani vikionekana kutelekezwa kwa siku nyingi sana. Rahab akalisogelea friji lililopo hapa sebleni kutazama kama kuna kitu chochote cha kuingiza mdomoni. Gafla kabla hajalifungua wakasikia mngurumo wa gari ukitokea kwa nje.
Wote kwa pamoja wakajikuta wakikimbilia dirishani kutazama ni kina nani walio wasili muda huu wa usiku. Wote wakajikuta wakiwa midomo wazi baada ya kuona watu wenye sura za kutisha zilizo kunjamana kunjamana wakishusha miili ya watu, walio fariki kwenye gari lao kubwa aina ya FYATA,  huku wakionekana kushangilia.
“Ni kina nani……!!?”
 
Rahab aliuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi usoni mwake
“Hata mimi siui ni kina nani”
Wakawashuhudia watu hao wakiingizwa kwenye moja ya kijumba kilichopo jirani na kijumba walipo wao, wakazidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona mtu mmoja kati ya hao wanao tisha akilitoa jicho la mmoja wa marehemu walio kuja nao na kuanza kulivyonza vyonza na taratibu akaanza kulila.
“Haaaaaa……!!!”
 
Rahab alimaka kwa sauti ya juu ila Raisi Pragod akawahi kumziba Rabab mdomno, sauti ya Rahab ikasikika moja kwa moja kwa mtu wa ajabu aliye kuwa anakula jicho la marehemu.
“Wametusikia tujifiche”
 
Raisi Praygod alizungumza huku akianza kung’aza ng’aza macho yake ndani kutafuta ni wapi wanaweza kujificha, hapakuwa na sehemu yoyote ya kujificha zaidi ya nyuma ya mlango, wote kwa pamoja wakasimama nyuma ya mlango na kujikausha kimya, mlango ukafunguliwa kwa nguvu na kuwabamiza kwenye vifua vyao huku, mtu huyo mwenye sura ya ajabu akiwa amesimama katikati ya mlango huku mkononi mwake akiwa ameshika bunduki aina ya gobore, huku macho yake akiyazungusha zungusha kila segemu ya seble hii.
                                                                                      ***
Kutokana na ujuzi mkubwa wa Samson katika kuendesha manohari pamoja na ndege, akaanza kazi ya kuibabadua manohari hii iliuyo ganda kwenye barabu kubwa katika bahari ya Atelantic, Ikawachukua masaa takribabani sita kuweza kuibabadua manohari hii ya kivita, inayo endelea kutafutwa na majeshi ya Tanzania wakisaidia na jeshi la Marekani, huku pia wakijitahidi kutafuta mabaki ya ndege ya muheshimiwa raisi bwana Praygod Makuya.
 
Taratibu wakaainaza safari huku Samson akiwapa kila mmoja majukumu yake katika kuifanya manohari hii kuweza kuendelea kupasua miamba ya barabu iliyopo kwenye bahari hii. Kadri jinsi walivyozidi kuiendesha ndivyo jisni walivyo zidi kufanikiwa kuweza kupasua miamba na kuzidi kwenda chini ya bahari ambapo hapakuwa na barafu kubwa sana.
 
Wakafanikiwa kufika kwenye ukanda ambao hauna barafu kabisa, ikawa ni kazi rahisi kwao kuendelea na safari yao. Furaha ikazidi kutawala ndani ya mioyo yao, huku Fety kila muda akionekana kuwaza kujua ni nini anapaswa kufanya.
“Jamani naomba tusikilizane”
 
Fety alizungungumza huku akiendelea kuwatazama wezake wanaoendelea kujiburudisha na vinywaji vikali vilivyomo ndani ya manohari hii.
“Tunakusikiliza kiongozi sema mama”
Agnes alizungumza kwa sauti iliyo jaa pombe
”Kurudi Tanzania hatuwezi, kwa sasa, kutokana tumekuwa ni maadui namba moja wa nchi hiyo”
 
“Sasa tutakwenda wapi, wakati Tanzania ndio nyumbani?”
Anna aliuliza huku akijitahidi kuyafumbua macho yake yalivyo zidiwa kwa pombe nyingi aliyo kunywa.
“Nimeona ni bora tukashauiriana kwenda kwenye nchi ambayo. Tutaomba hifadhi kwa muda huku tukikubaliana na serikali hiyo kuiuza hii manohari”
“Aisee wewe Fetty mbona unamaswala ya ajabu, hivi ni nchi gani ambayo itakubali kuuziwa hii manohari tena ya Tanzania. Hivi unajua kwamba Tanzani ina marafiki wengi kila kona ya dunia?”
 
Halima alizungumza huku akimkiendelea kushusha mapafu ya mzinga wa whyne alio ushika mkononi mwake. Fetty hakuwa na lakuzungumza ziadi ya kukaa kimya akiendelea kuyatafakari maneno aliyo yazungumza  Halima
“Ngoja niwashauri kitu ndugu zangu”
Samson alizungumza kwa sauti ya chini huku akiwatazama wote.
 
“Miimi nina rafiki zangu katika nchi ya Russia, ila wao ni waasi wan chi hiyo na wamejitenga kwenye moja ya kisiwa kilicho mbali kutoka katika nchi yao.”
“Ningependekeza kwamba kama tunahitaji kuweza kuiuza hii manohari, ni vyema kwenda walipo wao kisha tukazungumza nao bei, wakatupatia pesa kisha sisi tukatafuta sehemu ya maficho na kuendelea na maisha yetu ya kawaida”
“Hilo wazo nalo ni zuri, ila watu wenyewe kama ni waasi, kweli hawawezi kutubadilikia?”
 
“Mimi kiongozi wao mkuu ni rafiki yangu mkubwa sana, ambaye ni miongoni mwa watu walio nifundisha mimi kazi hii na kunipa ujuzi wa kuendesha vyombo mbalimbali vya kijeshi”
“Sawa, tutafikaje hapo?”
“Kutoka hapa tulipo sio mbali sana kikubwa ni kuweza kuamua kwamba tumekubaliana kwa pamoja kuweza kulitelekeza hilo, kisha mimi niweze kufanya mawasiliano na kiongozi wao”
 
Ukimya ukatawala kati yao huku kila mmoja akionekana kutafakari juu ya wazo la Samson, japo wote akili zao zina pombe kiasi ila kila mmoja alijitahidi kwa uwezo wake kuweza kuifuta pombe hiyo kichwani mwake na kuweza kutafakari kile alicho kisikia kutoka kwa Samson.
“Tutakuamini vipi kama huto tubadilikia hapo mbeleni?”
Fetty alimuuliza Samson huku akiwa amemkazia macho
“Niamnini, kwani nyinyi ni watu ambao mumuweza kunitendea mema na laity kama mungehitaji kunifanyia mabaya mungenisha nifanyia. Niwakati wa mimi kuweza kulipa wema kwenu”
 
“Sawa kama ni hivyo twendeni jamani, ,mimi nimeshachoka kukaa ndani yta maji kama samaki”
Halima alizungumza kwa msisitizo wote kwa pomoja wakakubaliana kuweza kulifwata wazo la Samson, Kila mmoja akajiegesha sehemu yake na kulala huku akisubiria masaa yakatize pombe ziwatoke kichwani waendelea na mpango wa kuwasiliana na hao watu wa Samson.
 
Anna akawa ni wakwanza kustuka, taratibu akanyanyuka huku akiwa amejawa na mawenge ya usingizi, akawatazama wezake, kwa mwendo wa kivivu vivu akaelekea chooni ambapo, alijisaidia haja ndogo kisha na kurudi walipo wezake.

 Akaanza kuwaamsha mmoja baada ya mwengine, walipo amka kila mmoja akaanza majukumu yake aliyo kuwa amekabidhiwa na Samson, kuhakikisha chombo hicho kimazidi kusonga mbele. 

Wakaanza kufanya mawasilianao na kikosi hicho cha kigaidi ambacho kimeiasi nchi yake ya Rusia. Kwa bahati nzuri wakafanikiwa kupata mawasiliano na kiongozi wa kikundi hicho aitwae Rusevu. 

Wakakubaliana naye kuweza kufika kwenye ngome yake siku mbili mbeleni wakiwa na manohari hiyo yenye uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi makubwa ndani ya maji. Mazungumzo ya Rusev na Samson yakazaa matumaini mapya ya utajiri kati ya Fetty na wezake kwani yote waliyo kuwa wakiyafanya ni kutokana na kuweza kupata pesa zitakazo wakimu kimaisha.
 
“Jamani kama hii dili, ikisimama mimi na ujambazi basi:
Fetty alizungumza, huku akiwa na furaha kubwa moyoni mwake
                                                                                                 *******
Mtu huyo wa ajaba akaendelelea kutazama tazama kila kona ya sable hii, akapiha hatua mbili mbele na kuzama ndani kabisa ya sable hii, na kuwapa mgongo Rahab na Raisi Praygod walio simama nyuma yake. 

Akaendelea kuvuta vuta pumzi, iliyo muashiria kwamba humu ndani kuna binadamu waklio hai, akalikoki bunduli lake aina ya gobore na kulishika vizuri huku kidole chake kimoja akiwa amekizamisha kwenye traiga, kwa haraka  akageuka nyuma na kuwaona Rahab na Raisi Praygod wakiwa nyuma yake wanamtazama


  ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Sponsor