Advertisement

Breaking

Wednesday, October 12, 2016

Tanzia: Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Masaburi afariki Dunia

Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amefikwa na umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.

“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa sijaenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.

Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Mtandao huu unatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu wa aliyekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa Amani. Amina!

No comments:

Post a Comment

Sponsor