Advertisement

Breaking

Monday, October 17, 2016

Watu 13 Kizimbani Kwa Mauaji ya Watafiti Dodoma


Wanawake wanne na wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjiniDodoma na kusomewa mashtaka ya mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi kilichopo Selian mkoani Arusha. 

Mbele ya Hakimu Mkazi, Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu. 

Wanadaiwa kuwaua Nicas Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi kwenye Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino. 

Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai walitenda kosa hilo la jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na marekebisho yake ya mwaka 2002. 

Washtakiwa hao ni Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma Madeha, Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga, Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba, wote wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi.

Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika. 

No comments:

Post a Comment

Sponsor