Advertisement

Breaking

Monday, November 7, 2016

TAKUKURU Yajitosa Kuchunguza Tuhuma za Wabunge wa CCM Kuhongwa Milioni 10

Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (Takukuru) imeanza kuchunguza tuhuma zilizoibuliwa Bungeni kuwa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipewa rushwa ya shilingi milioni 10.
 
Tuhuma hizo zilitolewa wiki iliyopita Bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe alipomuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 

Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
 
Mbowe alitaka kufahamu kutoka kwa Waziri Mkuu kama tuhuma hizo ni za kweli au la, akidai fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi kupitisha muswada wa sheria ya huduma za habari na mpango wa maendeleo ya taifa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imeanza uchunguzi kama alivyosema Rais John Magufuli alipokuwa akijibu swali katika mkutano wake na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita, Ikulu jijini Dar es Salaa.
 
“Ndiyo, tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chake na tumeanza kazi hiyo,” Mlowola anakaririwa .
 


Mkuu huyo wa Takukuru alifungua mlango kwa yeyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma hizo aziwasilishe ili kukisaidia chombo hicho.

No comments:

Post a Comment

Sponsor