Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa ukimya wa Rich Mavoko unatokana na msanii huyo kujipanga na kazi zake mwenyewe na kudai mpaka sasa amefanya kazi nyingi na kali sana.
Diamond Platnumz alisema hayo hivi karibuni kupitia kipindi cha Friday Night Live na kusema kuwa Rich Mavoko amefanya kazi nyingi lakini yeye mwenyewe anaziweka pembeni na kutaka kufanya kazi kali zaidi.
"Mimi mwenyewe nimefanya nyimbo nafikiri mbili na Richard na muda wowote zinaweza kutoka, sema Richard ni mtu fulani ambaye anajipanga hivyo kipindi hiki anajipanga akianza kufumuka na mabomu yake ni hatari, maana anajipanga kila wimbo akirekodi anakwambia hii bado, akirekodi nyingine tena anakwambia hii bado yaani naweza kusema Richard ni msanii ambaye ana nyimbo nyingi sana kali. Kuna wimbo pale unaitwa 'Sijaona' WCB nzima wanaikubali lakini yeye anakwambia hii bado, ila akisema hivyo akileta ngoma nyingine inakuwa kali zaidi. Kwa hiyo ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu kamjalia kipaji na mwenyewe anakuaga hana papara" alisema Diamond Platnumz
Thursday, November 3, 2016
Diamond Afunguka Kuhusu Ukimya wa Rich Mavoko
Tags
# Burudani
# Udaku
About Mina Ashelly
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Newer Article
Kwa Upuuzi Huu Nitaendelea Kuwasifu Mahausigeli Wanaovunja Ndoa za Watu!
Older Article
Watiwa Mbaroni Kwa kuvujisha mtihani FEKI wa kidato cha nne
Aunty Ezekiel amtemea ‘cheche’ Wema SepetuNov 22, 2016
Diamond Afunguka Kuhusu Ukimya wa Rich MavokoNov 03, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment