Advertisement

Breaking

Thursday, November 3, 2016

Kwa Upuuzi Huu Nitaendelea Kuwasifu Mahausigeli Wanaovunja Ndoa za Watu!

Kila siku na kila mahala ukipita au ukibahatika tu kukutana na akina Dada na akina Mama waliopo katika Ndoa au hata Mahusiano tu ' lawama ' zao kubwa ni kwa hawa Dada zetu wa Kazi nyumbani maarufu kama ' mabeki tatu ' kuwa wanashiriki kwa kiasi kikubwa sana katika kuwaharibia ' mahusiano ' yao kwa ' kubanduana ' na Wapendwa wao hasa Wachumba au Waume zao.

Kinachonisikitisha na hata kunishangaza pia ni Kitendo cha hawa hawa Dada / Mama zetu wao kuelekeza tu ' lawama ' zao kwa ' mahausigeli ' pasipo hata wao wenyewe ' kujitathmini ' ni wapi huwa wanakosea kwani ' kimantiki ' haiwezekani Mahusiano yao au Ndoa zao ziharibiwe bila sababu ' maalum '.

Katika chunguza chunguza yangu ya ' kutukuka ' kabisa ya kutaka kujua labda ' tatizo ' ni nini niliamua kulifuatilia ' kiumakini ' mno hili jambo na nikagundua mambo kadhaa ya ' kipuuzi ' ambayo Dada zetu walio katika Mahusiano au Mama zetu walio katika Ndoa zao huyafanya ambayo kwa kiasi kikubwa Mimi binafsi nawasapoti 100% ' mahausigeli ' kwani wanatumia ' upopoma wa kutukuka ' unaofanywa na hawa wenye Wachumba / Waume zao.

Mambo yenyewe ya ' kipuuzi ' ni kama yafuatayo:
Mama  anaenda kuajiri ' hausigeli ' mzuri kuliko hata yeye tena kwa kila kitu.
Mama  anaruhusu ' ukaribu ' wa ' kupitiliza ' wa Baba / Mchumba na ' Hausigeli '.
Mama  anamruhusu ' Hausigeli ' kuvaa ' vimini ' mbele ya Baba / Mchumba.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' amfulie ' Nguo ' Baba / Mchumba.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' awe na mazoea ya kuingia ' Master Bedroom '.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' aandae ' Chakula ' cha Baba / Mchumba huku yeye akiwa ' busy ' anatizama ' Isidingo ' na ' akitiririka ' na WhatsApp.

Mama anajifanya kuiga mambo ya ' kizungu ' kwa kuonyesha ' manjonjo ' yake ya ' Kimahaba ' tena mbele ya ' Hausigeli ' kitu ambacho huwafanya ' Mahausigeli ' wengi kuweza kuangalia ' udhaifu ' wao na pale Wao wakija ' kutongozwa ' tu akina Baba / Wachumba huwa hawakatai na ikifika wakati wa ' kubanduana ' huyu ' Hausigeli ' atamfanyia Baba / Mchumba ' manjonjo ' yake yote hivyo kumfanya kuonekana bora zaidi na hapo ndipo mwisho wa ' mahaba niue ' kwa akina Dada / Mama na kubaki kulaumu tu na kulia lia.

Wadada wa Kazi wote nchini Tanzania ' ninawasifu ' sana na nawaombeni endeleeni hivyo hivyo kuzitumia ' fursa ' hadi hawa akina Dada na Mama ' wakome ' na ' wanyooke ' kwa ' kuziharibu ' Ndoa zao / Mahusiano yao.

GENTAMYCINE

No comments:

Post a Comment

Sponsor