WATU
wanne wamekufa huku sita wakijeruhiwa katika ajali ya basi, lililogonga
lori katika eneo la njiapanda ya Kolandoto mkoani Mwanza.
Ajali
hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya JM Luxury kuligonga lori aina TATA,
lenye namba za usajiri T218 ABY, la Kampuni ya Birichand lililokuwa
likitoka mjini Shinyanga kwenda Kishapu.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa 11 .15 alifajiri jana.
Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi wa basi hilo lililokuwa likitoka Shinyanga kwenda Mwanza.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, watu wanne waliokufa walikuwa ndani ya lori, ambalo liligongwa na basi upande wa kulia.
Alisema
mbali na kuwa katika mwendo kasi, basi hilo lilitaka kulipita lori hilo
ambalo lilikuwa linaanza kukata kona kuelekea wilayani Kishapu, hivyo
kuligonga kwenye kichwa na kusababisha vifo hivyo.
Kamanda
Mwita hakutaja waliokufa katika ajali hiyo, lakini alisema miili yao
imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Majeruhi
wamelazwa hospitali hiyo na Hospitali ya Kolandoto. Alitaja majeruhi
wanne waliolazwa katika Hospitali ya Kolandoto kuwa ni Salehe Kassim
(46) ambaye ni dereva wa basi na Mohamed Ahmed (39) ambaye ni kondakta
wa basi.
Abiria
waliolazwa ni Valencia Magingi (34) aliyepo Hospitali hiyo ya Kolandoto
na waliolazwa Hospitali ya Mkoa ni Joseph Mkunda (58) na Salome Paulo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk George Herberth alikiri kupokea
majeruhi wawili ambao ni Salome Paulo aliyepata majeraha na kuvunjika
mguu wa kulia ambaye anaendelea na matibabu huku Joseph Mkunda akipata
matibabu na kuruhusiwa kuondoka. Miili ya waliokufa imehifadhiwa
hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment