MBUNGE wa Singida Mashariki
ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu,
amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa
Ibrahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga
wanachama wa CUF.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa
Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama
walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili
tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka
na viti 10.Mbunge wa Singida Mashariki
ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheia Mkuu
wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari.
Kauli hiyo ameisema jijini Dar es
Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba
aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai
ya kuwa kinaivuruga CUF.
Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa
matamshi hayo kwa wanachama wa CUF ni chanzo cha yeye kuendelea
kukivuruga chama hicho hivyo wanachama wampuuze kwani alikikimbia tokea
walipoungana katika umoja wao wa Ukawa kabla ya mwezi mmoja kujiunga
aliyekuwa mgombe urais kupitia umoja huo, Edward Lowasa kupitia Chadema.
Kwa
upande mwingine Lissu amesema viongozi wa Chadema wamepanga Jumanne
wiki ijayo kupelekea malalamiko yao katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa
ajili wafuasi 10 wa Chadema waliokamatwa kwa madai ya kusambaza maneno
ya uchochezi.Alisema wanapeleka hoja hiyo mahakamani ili mahakama iweze
kuamuru waachiwe huru kwani hivi sasa wanateseka mahabusu.
Alisema mahakama ndiyo chombo kikuu chenye dhamana ya kuwahoji Mkuu
Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini
DCI, Diwan Athumani ili watoe sababu ya jeshi la polisi kuwaweka
mahabusu wanachama 10 wa chadema kwa zaidi ya wiki moja sasa bila
kuwapeleka mahakamani.
No comments:
Post a Comment